Mwenyekiti wa TUCTA taifa Omary Ayub Juma
ameyasema hayo jijini Mbeya wakati akifunga mafunzo ya siku tano ya wafanyakazi
kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara yaliyokuwa yakiendeshwa katika chuo
cha wafanyakazi kilichopo jijini hapo.
Juma amesema kupitia makongamano hayo
licha ya wafanyakazi kujadili namna ya kukabililiana na changamoto mahala paa
kazi pia wataweza kujikumbusha wajibu wao hasa kwa kujifunza zaidi juu ya
sheria za kazi.
Aidha mwenyekiti huyo pia amesema TUCTA
inaangalia uwezekano wa kukiboresha chuo cha wafanyakazi Mbeya kutokana na
madhari yake kutoendana na hadhi yake.
Ameyasema hayo kufuatia wahitimu wa
mafunzo hayo kupitia risala iliyosomwa na mwenzao Sima Kazaula kuelezea
kutoridhishwa na hali ya majengo ya chuo wakisema yamechakaa na yanahitaji
maaboresho makubwa.
No comments:
Post a Comment