Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Monday, April 2, 2012

WANAVYUO WAASWA KUGOMA NA KUANDAMANA KWA MASLAHI YA TAIFA

WANAFUNZI wa Vyuo vikuu nchini wametakiwa kuandamana kwa ajili ya kutetea maslahi ya taifa badala ya kufanya hivyo kwa maslahi ya mtu binafsi au kikundi cha watu wachache.
Wito huo umetolewa na Dk. Steven Mwakajumilo wakati akiendesha Kongamano kubwa la wanafunzi wa vyuo vya elimu ya Juu lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) Jijini Mbeya.
Dk. Mwakajumilo amesema wanafunzi wa vyuo vikuu ni sehemu ya wasomi wanaoheshimika sana nchini na hivyo kabla ya kufanya jambo lolote wanapaswa kutafakari kwa kina faida na madhara ya jambo husika.
Anasema kuwa hata kama kuna kero inawahusu wanafunzi wenyewe lakini haina maslahi kwa taifa, hakuna sababu ya kuandamana barabarani na badala yake wanaweza kutumia njia nyingine kupata ufumbuzi badala ya kuandamana.
Katika kongamano hilo ambalo liliandaliwa na Serikali ya wanafunzi wa Chuo cha Teku, (Tekuso), mada kuu ilikuwa ni kujadili ‘changamoto za kimaendeleo Tanzania’ na  wahadhiri kutoka vyuo mbalimbali mkoani hapa walialikwa kwa ajili ya kutoa mada.

No comments:

Post a Comment