Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Saturday, April 7, 2012

YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI HALMASHGAURI YA WILAYA YA MBOZI

Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi wamehimizwa kutoa ushirikiano kwa watumishi wapya walioajiriwa na kupelekwa kwenye maeneo yao hivi karibuni katika sekta za Elimu na Kilimo.
Mkuu wa wilaya ya Mbozi GABRIEL KIMOLO akifungua mkutano wa baraza la madiwani Mbozi
Mkuu wa wilaya ya Mbozi Gabriel Kimolo ametoa hamasa hiyo alipokuwa akitoa salamu za serikali katika kikao cha kujadili bajeti cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri uliopo katika mji mdogo wa Vwawa.
 
Kimolo amesema madiwani wanapaswa kuwa mstari wa mbele kuionyesha jamii inayowazunguka kuwapa ushirikiano watumishi hao ambao wengi wao ni vijana na wanakabiliwa na changamoto mbalimbali katika maisha yao mapya ya utumishi.

Amesema ni vema madiwani wakachukua nafasi ya kuwa wazazi wa watumishi hao ili wajisikie wako nyumbani na kuwashirikisha katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto zozote zitakazo ibuka zikiwakabili .

wakati huohuo
SERIKALI wilayani Mbozi mkoani Mbeya imeelezea kuendelea vizuri na maandalizi ya kuanzisha benki ya wananchi ifikapo Julai mwaka huu.


MWENYEKITI wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi ERICK MINGA AMBAKISYE


Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya hiyo Gabriel Kimolo hadi sasa zaidi ya hisa zilizo na thamani ya shilingi milioni 582 zimeahidiwa kununuliwa na wananchi wilayani hapo hali inayoleta matumaini makubwa ya kufanikiwa kuanzishwa kwa benki hiyo.

Kimolo amesema kupitia uuzaji wa hisa kwa shilingi 1000 kila moja wilaya inatarajia kuanza na mtaji wa shilingi bilioni 2 hivyo watakuwa wamevuka kwa kiasi kikubwa sharti la kuanzisha benki ya wananchi la kuwa na fedha zisizopungua shilingi milioni 250.

Amesema pia uongozi bado unashughulikia kurejeshwa kwa shilingi 24 milioni ilizotoa ikiwa ni mchango wa kuanzisha benki ya wananchi mkoa lakini badaye kupitia kikao cha ushauri cha mkoa ikaonekana benki ya mkoa haitakuwa na msaada mkubwa kwa wananchi badala yake zikanzishwe katika kila wilaya.


Mkuu huyo wa wilaya amesema tayari imeundwa kamati maalumu inayosimamia uanzishwaji wa benki hiyo iliyopewa jina la Kamati Anzilishi inayoratibiwa na mmoja wa wataalamu kutoka chama cha ushirika cha Unyiha Association cha wilayani hapa Charles Chenza.

Hata hivyo amesema nguvu ya madiwani inahitajika kwa kiasi kikubwa katika kuwahamasisha na kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kuwa na benki yao na manufaa watakayoyapata.
 MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA MBOZI LEVISON CHILLEWA AKITOA UFAFANUZI JAMBO KWENYE KIKAO HICHO
SHILINGI milioni 40 za mfuko wa jimbo la Mbozi Magharibi zimeendelea kukaa benki bila matumizi kufuatia mwenyekiti wa mfuko huo mbunge David Silinde kutotaka kujihusisha kwa lolote juu ya matumizi ya fedha hizo.



Hali hiyo imeonekana kulisikitisha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi ambalo sasa limechukua uamuzi wa kutafuta namna ya kupata utaratibu mbadala utakaowezesha fedha hizo zitumike kwa maendeleo ya wananchi wa jimbo hilo.

Diwani wa kata Halungu Samson Simkoko ndiye aliyeibua hoja hiyo katika kikao cha baraza hilo akisema mbunge mekwamisha matumizi ya fedha hizo na kuomba atafutwe msimamizi mwingine atakayewezesha kutumika kwa fedha hizo

Naye diwani wa kata ya Msangano Omar Sinkala ameomba baraza kuazimia kumfikisha mahakamani mbunge Silinde kwa kukwamisha maendeleo ya wananchi.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Eliki Ambakisye amesema fedha hizo zilipaswa kugawanywa katika miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi lakini kutokana na mbunge kutofuatilia zimeendelea kukaa kama fedha zisizo na kazi.


No comments:

Post a Comment