Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Saturday, April 21, 2012

WAJASIRIAMALI WAPEWA MAFUNZO

WASHINDI 12 wa shindano la Safari Wezesha linaloendeshwa na Kampuni ya Bia nchini (TBL) kutoka mikoa ya nyanda za juu kusini wamepewa mafunzo ya ujasiliamali kabla ya kukabidhiwa vifaa vya kuwasaidia kuendeleza biashara zao kwa ufanisi.
Wakufunzi kutoka kampuni ya TIP ya Dar es Salaam ndiyo waliopewa dhamana ya kuendesha mafunzo hayo yaliyodumu kwa muda wa siku tano jijini Mbeya.

Mratibu wa mafunzo kutoka kampuni ya TBL, Onesmo Swila amesema washindi hao wanatarajiwa kuwezeshwa kwa kukabidhiwa vifaa hivyo Mei 26, mwaka huu.

Swila alifafanua kuwa jumla ya wajasiriamali 263 walijitokeza kushiriki shindano hilo kwa kujaza fomu za ushiriki kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.
Amesema baada ya fomu hizo kupitiwa, wajasiriamali 20 ndio waliokidhi vigezo vya kupewa msaada wa Safari Wezesha kwa ajili ya kusaidiwa kuendeleza biashara zao.


Mwenyekiti wa wajasiriamali hao katika mafunzo yao, Festo Sikagonamo amesema mafunzo hayo yaliyoanza tangu Aprili 16, mwaka huu yamewapa ujuzi na maarifa ya kuziinua biashara zao hata kabla ya kukabidhiwa vifaa vya Safari Wezesha.

No comments:

Post a Comment