VIONGOZI na
wajumbe wapya wa Baraza kuu la wafanyakazi wa shirika la hifadhi ya jamii (NSSF)
wametakiwa kufanya kazi kwa uadirifu
wakitambua fika kuwa nyuma yao wapo wafanyakazi wanaowategemea kuleta ufanisi
kiutendaji.
Waziri wa Kazi na
Ajira Gaudencia Kabaka amesisitiza hayo (April 18) wakati akifungua mkutano
wa 38 wa baraza kuu la wafanyakazi wa NSSF uliofanyika jijini Mbeya na
kuhudhuriwa na wajumbe mbalimbali kutoka ofisi za matawi yote ya shirika hilo.
Waziri Kabaka pia
amesisitiza shirika hilo kuona umuhimu wa kuendelea kuwekeza katika mikoa
mbalimbali iliyo na fursa za uwekezaji ikiwemo mkoa wa Mbeya hasa katika mradi
wa Makaa ya mawe wa Kiwira mara tu serikali itakapotoa maamuzi.
Awali mkuu wa mkoa
wa Mbeya Abbas Kandoro ameelezea kutoridhika na uwekezaji wa miradi ya
kimaendeleo unaofanywa na NSSF akisema mkoani Mbeya akisema bado haukidhi
ikilinganishwa na ilivyofanya kwa mikoa mingine.
Kandoro amesema
upo umuhimu mkubwa wa viongozi wa shirika hilo kufanya mazungumzo na uongozi wa
halmashauri ya jiji la Mbeya ili kufikia makubaliano ya kuweikeza katika miradi
ya ujenzi wa masoko ya kisasa pamoja na nyumba kwaajili ya makazi hasa
ikizingatiwa kuwa jiji hilo linakuwa kwa kasi ya asilimia 7.
No comments:
Post a Comment