Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Wednesday, April 4, 2012

MIDAHALO YA NKANGO YAAHIORISHWA MPAKA WABUNGE WARUDI MAJIMBONI


MIDAHALO miwili ya kuboresha mahusiano kati ya viongozi wa kuchaguliwa na wananchi wanaowaongoza iliyokuwa ifanyike wilayani hapa imeahirishwa.
Midahalo hiyo iliyoandaliwa na mtandao wa asasi za kiraia wilayani Nkasi mkoani Rukwa NKANGONET ilikuwa ifanyike katika kata ya Kirando jimbo la Nkasi Kaskazini na Kate jimbo la Nkasi kusini.

Mwenyekiti wa Mbengonet Victor Sadala akizungumza na waandishi wa habari,alisema midahalo ilipangwa kufanyika mwishoni mwa wiki jana lakini mkuu wa wilaya hiyo Joyce Mgana akashauri iahirishwe kutokana na wabunge wa majimbo hayo kuwa safarini kikazi.

Kwa mujibu wa Sadala mkuu huyo wa wilaya alishauri mikutano hiyo kufanyika pale wabunge hao watakapokuwa wamerejea na kubainisha kuwa hivi sasa wapo mjini Dodoma wanakohudhuria vikao vya bunge.

Hata hivyo mwenyekiti huyo hakubainisha ni lini mikutano hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na wananchi itafanyika lakini akasisitiza kuwa ni mara baada ya viongozi hao kurejea majimbo ni mwao.

“Tulimfuata mkuu wa wilaya ili tupate kibali cha kufanya midahalo yote miwili lakini akatushauri kwakuwa inalenga kuboresha mahusiano ni muhimu wabunge wawepo ili wapate moja kwa moja maoni ya wananchi wao”.

“Tumeona na wazo la msingi japo tayari sehemu kubwa ya maandalizi ilikuwa imefanyika.Lakini tukaona kwakuwa utawala wa wilaya umeshauri ni vema tukazingatia ushauri huo wa kuwa subiri wabunge kwa majimbo yote mawili”.

Kwa upande wake katibu wa Nkangonet Oscar Msangi aliwasihi wananchi kutokana tamaa kwa kuahirishwa kufanyika mikutano hiyo inayofadhiliwa na shirika la The Foundation For Civil Society na kusisitiza kuwa lazima itafanyika.
 Viongozi hao wamelazimika kutoa ufafanuzi huo kufuatia wakazi wa majimbo hayo kulalamikia kutofanyika kwa midahalo hiyo baada ya kuahidiwa ambapo pia wanaamini ni fursa ya kipekee ya kuwasilisha hoja zao kwa viongozi.

No comments:

Post a Comment