Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Wednesday, April 4, 2012

Nkasi yaomba serikali kuwawezesha waandishi wa habari kuwafikia

SERIKALI nchini imeshauriwa kuwawezesha waandishi wa habari kuyafikia maeneo ya pembezoni yaliyosahaulika na vyombo vya habari ni kuzifanya jamii za huko kukosa haki yao ya msingi ya kusema changamoto zinazowakabili.Nilipokutana na Leonard Sindani rafiki yangu mkubwa niliyesoma naye darasa la tatu hadi kidato cha nne lakinmwenzangu anafanya shughuli ya upigaji picha katika kijiji cha Nkundi wilayani Nkasi mkoani Rukwa
Ushauri huo umetolewa na mwenyekiti wa mtandao wa asasi zisizo za kiserikali wilayani Nkansi (Nkangonet) Victor Sadala ikiwa ni siku chache tangu rais kikwete kutaja changamoto mbalimbali zinazowakabili waandishi wa habari nchini katika utendaji kazi wao wa kila siku.

Sadala alisema bado wakazi wa maeneo ya pembezoni hawajanufaika na uwepo wa vyombo vingi vya habari kwakuwa hawapati fursa ya kuandikwa ama kutangazwa kupitia vyombo hivyo ikilinganishwa na wakazi wa maeneo ya miji mikubwa.

Aliitaja wilaya ya Nkasi kuwa miongoni mwa wilaya zisizopewa kipaumbele katika kurasa ama vipindi vya vyombo vya habari na kuifanya jamii husika kubaki ikiishi maisha yasiyojulikana kwa wengi.

Mwenyekiti huyo alisema wilaya ina matukio mengi yanayofaa kutangazwa lakini kutokana na uwezo mdogo kiuchumi walio nao wawakilisha wa vyombo vya habari wanashindwa kufika huko mara kwa mara.

Aliongeza kuwa badala yake wanahabari waofika wilayani hapa ni wale tu walioambatana na viongozi wa kiserikali ama vyama vya kisiasa na hapo wanalazimika kufuata ratiba za wakubwa hao na kukosa muda wa kuzungumza na wananchi kwa kina.

“Ni vigumu kwa mwanahabari anayekuja akiwa ameambatana na viongozi akakaa na mwananchi wa chini na kupata changamoto zetu kwa kina.Lazima atafuata ratiba ya kiongozi aliyekuja naye.Kwa hali hiyo maeneo wasiyopenda kwenda viongozi habari za huko hazitosikika siku zote” alisema.

Alifafanua kuwa kwa serikali kuwawezesha wanahabari kuyafikia maeneo ya pembezoni kunaweza kusaidia wana tasnia hiyo kuibua mambo mengi yaliyopo huko na kuleta msukumo kwa wadau mbalimbali kuyatafutia ufumbuzi.

No comments:

Post a Comment