SERIKALI wilayani Mbozi imesema itawachukulia hatua za kisheria watu wote watakaohusika na biashara ya kahawa mbichi katika msimu ujao wa mavuno ya zao hilo.
Mkuu wa wilaya
hiyo Gabriel Kimolo ametoa onyo hilo
leo alipotoa salamu za serikali katika kikao cha kawaida cha baraza la
madiwani.
Kimolo amesema licha
ya serikali kupitia wizara husika kutoa maamuzi yaliyotokana na ushauri wa
vikao halali vya serikali ya wilaya na mkoa kukataza ununuzi huo bado kuna watu
wana dhamira ya kukiuka agizo.
Amesema watu hao
wanajaribu hata kughushi barua na kuzituma kwa utawala wa wilaya na mkoa
kuarifu kuwa ununuzi wa kahawa mbichi umeruhusiwa na ofisi ya waziri mkuu jambo
ambalo halina ukweli.
Amesisitiza kuwa
mkono wa sheria katika uwajibishaji utawalenga wauzaji na pia wanunuzi wa
kahawa mbichi kwakuwa wote watakuwa wanakiuka agizo hilo.
No comments:
Post a Comment