Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Sunday, April 29, 2012

MBEYA WALIVYOSHEREHEKEA MIAKA 48 YA MUUNGANO WA TANZANYIKA NA ZANZIBAR KATIKA KIJIJI CHA CHALANGWA WILAYANI CHUNYA

 Baadhi ya wakuku wa wilaya za mkoani Mbeya waliohudhuria sherehe za muungano katika kijiji cha Chalangwa wiolayani Chunya wakifuatialia kwa makini hotuba ya kaimu mkuu wa mkoa Evance Balama ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Mbeya.
 Wananchi waliohudhuria sherehe za miaka 48 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Mmoja wa wanafunzi wa shule ya sekondari Chalangwa akijimwaga mbele ya watazamaji wakati wa ngonjera iliyoandaliwa na wanafunzi hao
Mambo ya KIDUKU hayakuachwa nyuma,Huyu ndo bingwa wa viduku kwa shule nzima ya sekondari Chalangwa
Mikogo,na jinsi alivyokuwa akimwaga tungo zake ilikuwa burudani kwa kila aliyefika uwanjani hapa
Wapiga ngoma nao walikuwa na mambo yao yaliyonogesha zaidi sherehe hizi 
Chifu wa kabila la Wasafwa akiimba shairi aliloliandaa kwaajili ya muungano
 Baadhi ya wananchi walishindwa kuficha hisia zao na kuamua kuingia uwanjani kuonesha makeke wakati bendi ya muziki wa asili wa kabila la wasafwa ikitumbuiza
Inaonesha utamu ulikolea mpaka mwananchi huyu akaamua atumie viungo vyake vyote kucheza muziki wa Kisafwa.

No comments:

Post a Comment