Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Monday, April 2, 2012

MAMBO YA AIRTEL NA WATOTO KUELEKEA PASAKA

Watoto wa wateja wa kampuni ya Airtel Tanzania wakijumuika kwa pamoja
na watoto wa wafanyakazi wa Airtel katika shamra shamra tamasha
maalum la watoto kuelekea kusheherekea sikukuu ya pasaka kwa michezo
mbali mbali kwa pamoja ambayo imefanyika katika kituo cha michezo ya
watoto kiitwacho Fun Sport ndani ya jengo la Qualty center Jijini
Dar-es-salaam kwa hisani ya Airtel.

Meneja mauzo wa kampuni ya Airtel Tanzania Bi.Hilda Nakajumo akikata
keki kwa pamoja na Watoto wa wateja wa kampuni ya Airtel Tanzania na
watoto wa wafanyakazi wa Airtel katika shamra shamra za kuelekea
sikukuu ya pasaka ambapo watoto hao walipata nafasi ya kucheza
michezo mbali mbali kwa pamoja ambayo imefanyika katika kituo cha
michezo ya watoto kiitwacho Fun Sport ndani ya jengo la Qualty center
Jijini Dar-es-salaam.

Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni ya Airtel Tanzania Bw.Irene Madeje
akizungumza na waandishi wa habari katika sherehe ya michezo kwa
Watoto wa wateja wa kampuni ya Airtel Tanzania na watoto wa
wafanyakazi wa kampuni hiyo katika shamra shamra za kusheherekea
sikukuu ya pasaka na kuendeleza uhusiano mzuri uliopo kati ya wateja
wa Airtel na wafanyakazi wa Airtel ambapo watoto hao walipata nafasi
ya kucheza michezo mbali mbali kwa pamoja ambayo imefanyika katika
kituo cha michezo ya watoto kiitwacho Fun Sport ndani ya jengo la
Qualty center Jijini Dar-es-salaam.
Watoto wakicheza mchezo wa kuendesha magari wakati wa tamasha maalum
la michezo kwa watoto lilioandaliwa na Airtel ili kutoa nafasi kwa
watoto wafanyakazi wa Airtel pamoja na watoto wa wateja wa Airtel
jijini Dar esa salaam kukutana na kucheza michezo mbali mbali kwa
pamoja , tamasha hilo lililofanyika katika kituo cha michezo ya
watoto kiitwacho Fun Sport ndani ya jengo la Qualty center Jijini
Dar-es-salaam kwa udhamini wa Airtel

KAMPUNI YA SIMU YA AIRTEL yaanza shamra shamra za sikukuu kwa kushereheka na watoto Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel yaanza shamrashamra za sikukuu
kwa kujumuika na watoto wa wateja wao jijini Dar es saalam ambapo
watoto zaidi ya 150 walipata nafasi ya kukutana pamoja jumamosi
mwishoni mwa wiki hii katika ukumbi wa Quality Center - Fun sports na
kufurahi kwa pamoja.
.
Watoto wa wateja wa kampuni ya Airtel Tanzania wakijumuika kwa pamoja
na watoto wa wafanyakazi wa Airtel kukakata keki iliyoandaliwa na
kampuni ya Airtel Tanzania katika shamra shamra za tamasha maalum
kuelekea sikukuu ya pasaka ambapo watoto hao walipata nafasi ya
kucheza michezo mbali mbali kwa pamoja ambayo imefanyika katika
kituo cha michezo ya watoto kiitwacho Fun Sport ndani ya jengo la
Qualty center Jijini Dar-es-salaam.

Huu ni mkakati ambao Airtel imejiwekea kusherehekea pamoja na watoto
wa wateja wao wa makapuni ( corporate customer) wiki moja kabla ya
sikukuu za pasaka huku lengo likiwa ni kuwa karibu na wateja wao na
kusambaza upendo wa kampuni hiyo kwa wateja wake na familia zao.

Akiongea kwa niaba ya Airtel Mkurugenzi wa Biashara wa Airtel Bi Irene Madege
alisema" leo tunajisikia furaha kuwa na watoto wa wateja wetu na
kujumuika nao pamoja, Tumekuwa tukifanya shughuli mbalimbali ikiwa ni
katika kuwazawadia wateja wetu, lakini leo tunatumia muda huu kuwapa
burudani watoto ambao ndio wateja wetu wa kesho".

Kwa muda wa takribani masaa 4 watoto zaidi ya 150 walipata burudani
mbalimbali ikiwa pamoja na michezo mbalimbali ya watoto kama face
painting, mashindano ya kucheza music, na pia kupata nafasi ya
kukutana na wafanyakazi wa Airtel, kumzungumza pamoja na kuwasisitiza
watoto kuwa wasikivu shuleni ili kufanya vizuri kwenye masomo yao,
tunaamini watoto hawa wamekuwa na wakati mzuri pamoja nasi. Anaendelea kufafanua

No comments:

Post a Comment