Friday, January 8, 2016
KIWANDA CHA KUTENGENEZA SABUNI CHA HI SOAP MBEYA SASA CHAANZA KULIMA BANGI
Sehemu ya mimea ya bangi ikiwa imepandwa pamoja na maharage ndani ya eneo la kiwanda cha sabuni cha Hi Soap jijini Mbeya kama ilivyokutwa na wanachama wa Chama cha waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania(TAJATI).Kiwanda hiki kimetelekezwa kwa zaidi ya miaka 10 sasa na haijulikani mwekezaji yupi alibinafsishiwa
Sunday, January 3, 2016
FISTULA BADO NI TATIZO MBEYA!
HAMASA
ndogo juu ya matibabu ya Ugonjwa wa Fistula imetajwa kuwa chanzo cha jamii
inayosumbuliwa na ugonjwa huo kutojitokeza ili kupata matibabu.
Kaimu
mkuu wa Kitengo cha wazazi cha Meta katika Hospitali ya Rufaa kanda ya Mbeya Dk.Godlove
Mbwanji amebainisha hayo alipozungumza na waandishi wa habari juu ya mweneno wa
utoaji huduma kwa wagongwa wa Fistula.
Dk.Mbwanji
amesema uchunguzi unaonesha kuwa katika kipindi inapofanyika kampeni kubwa za
matibabu ya ugonjwa wa Fistula ambao kimsingi hutolewa bure ndipo wagonjwa
wengi hujitokeza kutibiwa na mara kampeni zinapokoma wagonjwa hujitokeza kwa
kusuasua.
Amesema
mwendo huo unatoa majibu yenye uhalisia kuwa wanawake wanaosumbuliwa na Fistula
ni wengi miongoni mwa jamii lakini hawafiki kupata matibabu kutokana na
kutokuwa na uelewa wa kutosha juu ya ugonjwa huo.
Asema
katika jamii bado kuna watu wanaojua ugonjwa huo hauna tiba,wengine hujua tiba
hutolewa kwa malipo na hivyo wanaogopa gharama huku wengine pia wakiuhusisha
ugonjwa huo na imani za kishirikina.
Amesema
ni vema kampeni za kuwaongezea uelewa wananchi katika maeneo mbalimbali juu ya
ugonjwa wa Fistula zikawa endelevu ili kuwezesha jamii kutambua kuwa ni ugonjwa
unaotibiwa bure na hata wagonjwa wanaofika hurejeshewa nauli waliyojia kwa hisani
ya shirika la kimataifa llinalojisgughulishaa na masuala ya Afya ya uzazi la
Amref.
Aidha,Dk.Mbwanji
ameyataja maeneo ya pembezoni kuwa yenye kusumbuliwa kwa kiasi kikubwa na Fistula
huku Kwa mkoani Mbeya akizitaja wilaya za Mbozi,Momba na Chunya kuwa zilizo na
wagonjwa wanaojitokeza kwa wingi kutibiwa ugonjwa huo.
Friday, January 1, 2016
TANZIA TANZIA TANZIA
Mhariri mkuu wa Blogu ya Lyamba Lya Mfipa Bwana
Joachim Nyambo,anasikitika kutangaza kifo cha mjomba yake Nickas Nkana
kilichotokea usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Tumbi iliyopo mkoani
Pwani.Safari ya kusafirisha mwili wa marehemu kuelekea Sumbawanga mkoani Rukwa
inatarajiwa kuanza wakati wowote mara baada ya taratibu za usafiri kukamilika.
Habari ziwafikie,ndugu,jamaa na marafiki wote.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa,jina la bwana na
libarikiwe!
Subscribe to:
Posts (Atom)