HAMASA
ndogo juu ya matibabu ya Ugonjwa wa Fistula imetajwa kuwa chanzo cha jamii
inayosumbuliwa na ugonjwa huo kutojitokeza ili kupata matibabu.
Kaimu
mkuu wa Kitengo cha wazazi cha Meta katika Hospitali ya Rufaa kanda ya Mbeya Dk.Godlove
Mbwanji amebainisha hayo alipozungumza na waandishi wa habari juu ya mweneno wa
utoaji huduma kwa wagongwa wa Fistula.
Dk.Mbwanji
amesema uchunguzi unaonesha kuwa katika kipindi inapofanyika kampeni kubwa za
matibabu ya ugonjwa wa Fistula ambao kimsingi hutolewa bure ndipo wagonjwa
wengi hujitokeza kutibiwa na mara kampeni zinapokoma wagonjwa hujitokeza kwa
kusuasua.
Amesema
mwendo huo unatoa majibu yenye uhalisia kuwa wanawake wanaosumbuliwa na Fistula
ni wengi miongoni mwa jamii lakini hawafiki kupata matibabu kutokana na
kutokuwa na uelewa wa kutosha juu ya ugonjwa huo.
Asema
katika jamii bado kuna watu wanaojua ugonjwa huo hauna tiba,wengine hujua tiba
hutolewa kwa malipo na hivyo wanaogopa gharama huku wengine pia wakiuhusisha
ugonjwa huo na imani za kishirikina.
Amesema
ni vema kampeni za kuwaongezea uelewa wananchi katika maeneo mbalimbali juu ya
ugonjwa wa Fistula zikawa endelevu ili kuwezesha jamii kutambua kuwa ni ugonjwa
unaotibiwa bure na hata wagonjwa wanaofika hurejeshewa nauli waliyojia kwa hisani
ya shirika la kimataifa llinalojisgughulishaa na masuala ya Afya ya uzazi la
Amref.
Aidha,Dk.Mbwanji
ameyataja maeneo ya pembezoni kuwa yenye kusumbuliwa kwa kiasi kikubwa na Fistula
huku Kwa mkoani Mbeya akizitaja wilaya za Mbozi,Momba na Chunya kuwa zilizo na
wagonjwa wanaojitokeza kwa wingi kutibiwa ugonjwa huo.
No comments:
Post a Comment