Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Wednesday, May 31, 2023

MAHUNDI AWAPA SAPOTI MWANJELWA VETERANI

 
Naibu waziri wa maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi amewapa sapoti ya vifaa mbalimbali wachezaji soka wa zamani wa Mwanjelwa Veterani kuelekea Bonanza la  maveterani  Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ambalo limepangwa kufanyika Juni tatu na nne mwaka huu.


Kwa mwaka huu mashindano hayo yatafanyika jijini Mbeya kwenye uwanja wa Magereza na uwanja wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya(Must).

 

Mwenyekiti wa Mwanjelwa Veterani Ndambi Mwaipopo amesema wao kama wenyeji wa mashindano hayo wanamshukuru Naibu waziri wa maji Mahundi kwa kuendelea kuwaunga mkono wachezaji waliocheza soka zamani maarufu kama maveterani ambao wamekuwa wakikutana mara kwa mara.

 

“Tunamshukuru sana Mhandisi Mahundi amekuwa bega kwa bega kusapoti michezo,mabonanza haya yanatukutanisha wachezaji wakongwe,tunabadilishana uzoefu wa mambo mbalimbali"amesema Mwaipopo

 

Mwanjelwa Veterans ndio mabingwa watetezi wa michuano hiyo ambapo msimu uliopita walifanikiwa kuchukua ubingwa wa Bonanza hilo ambalo lilifanyika Songea na Ilula.

 

CREDIT TO SHABAN NASSORO

PRISONS YAPIGA MARUFUKU WACHEZAJI NDONDO CUP

Klabu ya Soka ya Tanzania Prisons imepiga marufuku wachezaji wake kucheza michezo ya ligi za mchangani maarufu kama Ndondo Cup katika kipindi hiki cha kuelekea kumalizika kwa msimu wa ligi kuu ya NBC 2022/23.

 

Ofisa habari wa Prisons, Jackson Mwafulango amesisitiza kuwa ni marufuku wakati ligi ikiwa bado haijamalizika mchezaji wao kuchezea ndondo Cup na kusisitiza kuwa mchezaji yeyote atakaebainika atachukuliwa hatua za kisheria.

 

CREDIT TO SHABAN NASSORO


Tuesday, May 30, 2023

ZILIZOFUZU NUSU FAINALI AESHI SUPER CUP 2023

 


KUTOKA SUMBAWANGA- AESHI SUPER CUP 2023

 


MWENENDO WA AESH SUPER CUP- SUMBAWANGA.

 


KENGOLD KUVUNJA KIKOSI CHOTE, BENCHI LA UFUNDI


Mkurugenzi wa kikosi cha KenGold FC Keneth Mwakyusa Mwambungu amepanga kufanya maboresho makubwa katika timu hiyo kuelekea msimu ujao wa ligi ya Championship...!!

Mwambungu amesema baada ya kumalizika ligi wamefanya tathimini na kubaini mapungufu mbalimbali hivyo wanaanza kuyafanyia kazi mapema....!!
""Unajua ligi daraja la kwanza ni ngumu sana,,tumecheza huu msimu wa tatu sasa,,navunja kikosi chote pamoja na benchi la ufundi,tunaanza upya" Amesema Keneth
Nae Katibu mkuu wa KenGold Benson Mkocha ameongeza kuwa baada ya kushindwa kufikia malengo ya kupanda ligi wameona waanze upya ambapo hivi karibuni wataanza kutangaza utaratibu wa namna gani watafanya usajili...

MBEYA KUZIDI KUZALISHA VIPAJI VYA SOKA.

 Mwenyekiti wa Chama cha mpira wa miguu mkoa wa Mbeya(MREFA) Sadiki Jumbe amesema mkoa wa Mbeya umejaaliwa vipaji hivyo watahakikisha soka linachezwa kila sehemu...!!

Jumbe ameyasema hayo wakati wa Hafla ya utambulisho wa mashindano ya MO Quality Mbeya Ndondo Cup ambapo amesema kupitia mashindano hayo wanaamini wataibua vipaji ambavyo vitakuwa msaada kwa soka la Tanzania...!
""Mkoa wa Mbeya ni wa pili kisoka ukiondoa Dar es Salaam,tuna timu tatu za ligi kuu,tunatamani kuona hizi ndondo zinachochea maendeleo katika soka," amesema Jumbe
Mashindano ya MO Quality Mbeya Ndondo Cup 2023 yamepangwa kuanza kutimua vumbi June 10,2023 katika uwanja wa shule ya msingi Mwenge ambapo timu 16 zitashiriki michuano hiyo...!!




Saturday, May 20, 2023

HAKUNA MCHEZAJI ANAEDAI MSHAHARA MBEYA CITY


Mstahiki Meya wa jiji la Mbeya Dour Issa Mohamed ambae pia ni mlezi wa klabu ya Mbeya City amesema hakuna mchezaji yoyote anayedai mshahara kama inavyoripotiwa na baadhi ya wadau wa soka...!!

Ameyasema hayo wakati Taasisi ya Tulia Trust ikizindua zoezi la ugawaji wa jezi za mashabiki wa Mbeya City kutoka Kata zote 36 ndani ya jiji la Mbeya kwa lengo la kuhamasisha michezo....!!
""Maneno yamekuwa mengi ,,niwahakikishie wachezaji wamelipwa mpaka mwezi wa nne 2023 hakuna mchezaji anaedai mshahara,hata bonasi zao zote wamelipwa,,wale vijana wanafanya kazi wanafamilia zinawategemea kwaio lazima tuwawekee mazingira mazuri,tunathamini sana jasho lao"" amesema Dour Mohamed..
Hata hivyo ameongeza kuwa wadau na mashabiki wanapaswa kushikimana ili kuhakikisha kikosi chao kinamaliza vizuri michezo yao miwili iliyosalia ya kumaliza msimu wa mwaka 2022/2023 dhidi ya Yanga pamoja na KMC.

Friday, May 5, 2023

TFF YATUPILIA MBALI MAOMBI YA FEISAL JUU YA YANGA.

 


TANZANIA YACHAGULIWA KWA KISHINDO KUWA MAKAO MAKUU YA BARAZA LA MICHEZO AFRIKA KANDA YA NNE


 Na Mwandishi Wetu, Arusha.

 

Nchi Wanachama wa Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Kanda ya IV zimeichagua  Tanzania kuwa  Makao Makuu ya Sekretarieti ya Baraza hilo linaloundwa na nchi 14.

 

Ushindi huo umepatikana kupitia mkutano wa Baraza hilo uliofanyika jana Mei 4, 2023 jijini Arusha chini ya uongozi wa na Mwenyekiti  Mhe. Peter Ogwang ambaye ni Waziri anayeshughulikia masuala ya Michezo nchini Uganda.

 

Tanzania imepitiswa na Wajumbe kutoka Nchi 14 zinazoshiriki Mkutano  huo ambazo ni Comoro, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Madagascar, Mauritius, Rwanda, Shelisheli, Somalia, Sudan Kusini, Sudan, Uganda na  wenyeji Tanzania.

 

Akizungumza mara baada ya Tanzania kuchaguliwa, Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amewashukuru Wajumbe hao akiwahakikishia kuwa Tanzania itakua tayari kusimamia, kuendeleza na kuhakikisha mipango na matarajio ya Baraza hilo yanafikiwa kwa mafanikio makubwa.

 

Mkutano unaofuata wa Baraza hilo utafanyika Zanzibar Aprili, 2024.


WCB KUPAMBA KILELE CHA TULIA TRUST MARATHON 2023


Wasanii kutoka kundi la WCB wakiongozwa na Nasib Abdul maarufu kama Dimond Plutnamz kesho wanaungana na wasanii wengine katika kuyapamaba mashindano ya mbio ya Tulia Marathon 2023 ambayo yaliyoanza jana.

Kwa mujibu wa Mkuu wa kitengo cha Habari na mawasiliano cha Tulia Trust ,Joshua Mwakanolo wasanii wengine watakaoongozana na Dimond kutoka WCB ni Raymond Mwakyusa(Rayvan), Zuhura Othman Soud(Zuchu) na Mbwana Yusuph Kilungi(Mbosso)