Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Wednesday, May 31, 2023

MAHUNDI AWAPA SAPOTI MWANJELWA VETERANI

 
Naibu waziri wa maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi amewapa sapoti ya vifaa mbalimbali wachezaji soka wa zamani wa Mwanjelwa Veterani kuelekea Bonanza la  maveterani  Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ambalo limepangwa kufanyika Juni tatu na nne mwaka huu.


Kwa mwaka huu mashindano hayo yatafanyika jijini Mbeya kwenye uwanja wa Magereza na uwanja wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya(Must).

 

Mwenyekiti wa Mwanjelwa Veterani Ndambi Mwaipopo amesema wao kama wenyeji wa mashindano hayo wanamshukuru Naibu waziri wa maji Mahundi kwa kuendelea kuwaunga mkono wachezaji waliocheza soka zamani maarufu kama maveterani ambao wamekuwa wakikutana mara kwa mara.

 

“Tunamshukuru sana Mhandisi Mahundi amekuwa bega kwa bega kusapoti michezo,mabonanza haya yanatukutanisha wachezaji wakongwe,tunabadilishana uzoefu wa mambo mbalimbali"amesema Mwaipopo

 

Mwanjelwa Veterans ndio mabingwa watetezi wa michuano hiyo ambapo msimu uliopita walifanikiwa kuchukua ubingwa wa Bonanza hilo ambalo lilifanyika Songea na Ilula.

 

CREDIT TO SHABAN NASSORO

No comments:

Post a Comment