Na Mwandishi Wetu, Arusha.
Nchi Wanachama wa
Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Kanda ya IV zimeichagua Tanzania kuwa
Makao Makuu ya Sekretarieti ya Baraza hilo linaloundwa na nchi 14.
Ushindi huo umepatikana
kupitia mkutano wa Baraza hilo uliofanyika jana Mei 4, 2023 jijini Arusha
chini ya uongozi wa na Mwenyekiti
Mhe. Peter Ogwang ambaye ni Waziri anayeshughulikia masuala ya Michezo
nchini Uganda.
Tanzania imepitiswa na
Wajumbe kutoka Nchi 14 zinazoshiriki Mkutano
huo ambazo ni Comoro, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Madagascar,
Mauritius, Rwanda, Shelisheli, Somalia, Sudan Kusini, Sudan, Uganda na wenyeji Tanzania.
Akizungumza mara baada
ya Tanzania kuchaguliwa, Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt.
Pindi Chana amewashukuru Wajumbe hao akiwahakikishia kuwa Tanzania itakua
tayari kusimamia, kuendeleza na kuhakikisha mipango na matarajio ya Baraza hilo
yanafikiwa kwa mafanikio makubwa.
Mkutano unaofuata wa
Baraza hilo utafanyika Zanzibar Aprili, 2024.
No comments:
Post a Comment