Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Sunday, February 10, 2013

WAPELEKWA SEKONDARI KUJAZA VYUMBA

ASILIMIA 70 ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari mwaka huu wilayani Mbozi mkoani Mbeya hawana sifa za stahili za kujiunga na kidato cha kwanza. Asilimia hiyo ni ya wanafunzi 2,276 walioteuliwa kuingia kidato cha kwanza katika shule za sekondari za wilayani hapa kati yao wakiwamo wasichana 1,143 na wavulana 1,133. Mkuu wa wilaya ya Mbozi Dk.Michael Kadege aliyasema hayo katika kikao cha balaza la madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo na kuwataka madiwani na wadau wengine kuangalia ni namna gani wanaweza wakainusuru elimu wilayani kwao. Dk.Kadege alisema Utafiti uliofanywa umebaini kuwa kati ya wanafunzi hao waliochaguliwa hawakupata alama za ufaulu za A,B na C badala yake ililazimu kuchukua kuanzia waliopata alama D hadi F ili kupata wanafunzi wa kujaza mvyumba katika shule za sekondari.

No comments:

Post a Comment