Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Thursday, October 26, 2023

KenGold wataka kujiimarisha zaidi kileleni Championship



 

NA MWANDISHI WETU


VINARA wa NBC Championship League KenGold FC wamewasili salama mkoani Kagera kwa ajili ya mchezo wao wa mzunguko wa nane dhidi ya Biashara United uliopangwa kuchezwa katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba Jumamosi ya Oktoba 28,2023.

Vinara hao wamesema matarajio yao ni kuendeleza ushindi kwenye michezo yake ili kujiweka mahali salama zaidi hivyo wamejipanga kupata matokeo ya ushindi katika mchezo huo wa kesho.

Akizungumza kwa njia ya simu mara baada ya kuwasili Kagera mshambuliaji wa kikosi hicho, Emanuel Mpuka alisema licha ya kusafiri umbali mrefu wachezaji wote wapo na afya njema na morali kubwa kuelekea kwenye mchezo huo.

Aamesema matarajio ya matokeo bora yanatokana na maandalizi waliyoyafanya hata kabla ya kuanza kwa safari huku akisema mabadiliko ya hali ya hewa hayatarajiwi kuwa kikwazo kwao.

"Tunaamini kwenye maandalizi tuliyojiandaa, tumekuja kupambana kusaka alama tatu,hali ya hewa ya huku inautofauti mkubwa sana na Mbeya...kuna muda joto,kuna muda baridi na wakati mwingine mvua inanyesha kabisa. Lakini hiyo haituondoei kwenye nia yetu" Amesema Mpuka

Mshambuliaji huyo mpaka sasa amefunga magoli 3 na Assist 2 kwenye kikosi cha KenGold FC ambacho kinaongoza msimamo wa NBC Championship League kikiwa na alama 16.

No comments:

Post a Comment