Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Saturday, May 25, 2013

UMISSETA MBEYA YAMALIZIKA

MASHINDANO ya umiseta kwa shulea za sekondari(Umisseta) mkoa wa Mbeya yamemalizika na kupatikana wanafunzi 135 ambao watachujwa na kubakia 125 watakaounda timu ya mkoa kushiriki hatua ya kanda. Akitangaza matokeo ya mashindano hayo,afisa michezo mkoani hapa George Mbijima alisema katika mchezo wa mpira wa mkono(Handba ll) mshindi kwa wasichana ilikuwa halmashauri ya wilaya ya Mbozi na wavulana halmashauri ya jiji la Mbeya. Voleyball wasichana ilishinda halmashauri ya wilaya ya Mbeya na wavulana ikaibuka halmashauri mpya ya Busokelo huku mchezo wa Netiball wilaya ya Kyela wakiibuka mabingwa. Mchezo wa kikapu Rungwe alichukua kombe la ubingwa kwawasichana na wavulana jiji la Mbeya likaibuka kinara huku riadha Rungwe wakionesha kuwa mabingwa wa kukimbiza upepo. Mchezo wa fainali wa mpira wa miguu wavulana ulimalizika kwa vijana wa jiji kuwanyuka goli 2-1 wenzao wa Mbozi huku halmashauri ya wilaya ya Rungwe ikijilaumu yenyewe kwa kuchezesha mamluki hali iliyosababisha kunyang’anywa pointi sita ilizokuwa imepata kwenye michezo miwili ya awali. Hata hivyo wasichana wa halmashauri hiyo wakapunguza majonzi kwa kuibuka mabingwa kwenye mchezo wa soka pamoja na mpira wa meza ambao kwa wavulana mabingwa ni halmashauri ya jiji. Akifunga mashindano hayo afisa elimu mkoa wa Mbeya Juma Kaponda aliwataka waratibu kuhakikisha wanatafuta vikombe vyenye hadhi kwa washindi wa mwakani tofauti na vile vilivyotolewa mwaka huu. Kaponda alisema vikombe vya sasa havina hadhi ya mashindano ya sekondari kwani vinazidiwa hata na vile vya mashindano ya shule za msingi(Umitashumita) alivyosema ni vizuri na vina heshima ya mabingwa. Afisa elimu huyo aliagiza pia wakuu wa shule kutowaruhusu wanafunzi walio kidato cha nne la sita kushiriki mashindano hayo kwakuwa muda huo wanapaswa kujiandaa na mitihani sawa na ilivyo kwa wanafunzi wa darasa la saba kwa mashindano ya shule za msingi

No comments:

Post a Comment