Tuesday, May 28, 2013
COCA COLA WAPANIA KUCHEZA LIGI KUU
Meneja wa kiwanda cha Coca Cola Kwanza cha mkoani Mbeya Gary Pay akiwa amembeba mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda hicho ikiwa ni moja ya michezo iliyofanyika kwenye hafra ya kusherehekea kombe la mashindano ya kombe la
Mkurugenzi mkuu wa Coca Cola nchini lililofahamika kama MD Cup 2013
ambapo timu ya Coca Cola kwanza waliibuka mabingwa na kukabidhiwa
kombe hilo.
KIWANDA cha vinywaji baridi cha Coca Cola Kwanza cha mkoani Mbeya
kimeelezea nia yake ya kuwa na timu itakayoshiriki mashindano makubwa
nchini ikiwemo ligi kuu ya Tanzania bara.
Meneja wa kiwanda Gary Pay alieleza nia hiyo kwa wafanyakazi wake
waliohudhuria hafra ya kusherehekea kombe la mashindano ya kombe la
Mkurugenzi mkuu wa Coca Cola nchini lililofahamika kama MD Cup 2013
ambapo timu ya Coca Cola kwanza waliibuka mabingwa na kukabidhiwa
kombe hilo.
Pay alisema kampuni ya Coca Cola kupitia kiwanda hicho iko katika
mkakati wa kuhakikisha wanaismarisha timu hiyo na kuiwexzesha
kushiriki mashindano makubwa.
Alisema ili kutekeleza nia hiyo tayari kampuni imeingia mkataba wa
mwaka mmoja na kocha Charles Makwaza atakayekuwa akiinoa kwa muda huyo
na tayari wameanza mchakato wa kuisajili na kuiwezesha kushiriki
michuano kwa ngazi mbalimbali ili kuanza kupanda daraja.
“Sisi tunalinganisha uwepo wa timu sawa na utendajui katika kiwanda
chetu.Tukiitazama safu ya ushambuliaji ni sawa na safu yetu ya
mauzo,kwa upande wa safu ya ulinzi ni sawa na kitengo cha uzalishaji
kiwandani.Kwa ujumla timu yote ni sawa na watumishi wote pale
kiwandani.Hii ni sehemu ya mafanikio yetu kibiashara”
“Tumedhamiria,tumeamua na tunaamini tutafanikiwa siku moja kuwa na
timu itakayokuwa na upinzani mkubwa kwa timu nyingine nchini kwenye
mashindano makubwa hususani ligi kuu” alisema.
Naye kocha Makwaza alisema aliipongeza kampuni hiyo kwa kutambua uwezo
wake na kumpa mkataba wa kuifundisha timu hiyo huku akiahidi
kuhakikisha kikosi chake kinakuwa tishio kwa timu nyingine ili
kutimiza malengo ya kuanzishwa kwa timu.
Kwa upande wake nahodha wa timu hiyo Bahati Jonas alisema ushirikiano
wa karibu baina ya wachezaji na uongozi wa kampuni ni miongoni mwa
mambo yatakayoiwezesha kufikia malengo yanayotarajiwa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment