MKAZI wa kata ya Nzovwe,Jijini Mbeya,Rehema Mwamengo (39)
amependekeza katika katiba ijayo iwe na sheria ya kuhasiwa sehemu za siri kwa
mwanaume yoyote atakaebainika na kuthibitishwa na mahakama kumbaka mtoto wa
kike.
Kufuatia pendekezo hilo, umati mzima wa watu uliokuwepo
ukisikiliza mkutano huo kuangua kicheko huku wanawake wakionekana kupiga
vigelegele na makofi kwa kumsifu mama huyo.
Pendekezo hilo alilitoa mbele ya jopo la wajumbe wa tume ya
mabadiliko ya katiba mpya wakati wa mkutano wa kukusanya maoni toka kwa
wananchi juu ya mchakato mzima wa
uundwaji katiba nyingine itakayokuwa imewashirikisha wananchi kote nchini.
Mwamengo alisema kuwa hivi sasa adhabu ya mwanaume anayekutwa
na hatia ya kubaka kufungwa jela miaka 30 haitoshi kwa dai kuwa vitendo hivyo
bado vinashamili siku hadi siku miongoni mwa jamii.
Alisema kuwa vitendo hivyo licha ya kuwa na adhabu hiyo ya
kufungwa miaka 30 jela lakini watoto wanaokuwa wamefanyiwa kitendo hicho hujikuta
wakiwa katika hali mbaya ambapo baadhi yao hupata ulemavu sehemu za uzazi.
Aidha, alidai kuwa endapo katiba ijayo itaridhia kuwepo kwa
adhabu hiyo ya kuhasiwa kwa mwananume anayekuwa na hatia ya kubaka heshima itakuwepo
na itakuwa ni fundisho hata kwa wale wenye tabia ya kupalamia watoto wa kike.
“Nasema hivi mwanaume yoyote atakakaebainika na kuthibitishwa
na mahakama kuwa ana hatia hiyo ya kubaka adhabu yake iwe ni kuhasiwa tu ili
iwe ni fundisho kwa wanaume wengine”alisema mama huyo na kuongeza:
“Hivi sasa adhabu ya
mwanaume atakaekutwa na hatia kama hiyo kufungwa miaka 30 na adhabu hiyo
inatekelezwa na mahakama lakini bado tabia hiyo ipo na inazidi kuwaumiza mabinti
zetu, na hali hiyo inaashilia kuwa haitoshi kwa mwanaume huyo,hivyo
nashauri kwamba adhabu yake iwe ni kuhasiwa tu”alisema.
No comments:
Post a Comment