Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Friday, November 30, 2012

TBL,WANAHABARI TULIPOAMUA KUPIMA HIV KATIKA ZOEZI MAALUMU LA KUPIMA AFYA ZA WAFANYAKAZI KATIKA KIWANDA TBL MBEYA

 Alianza Meneja wa kiwanda hicho Nicholaus Kanyamala kama anavyoonekana hapa

 Akafuata mfanyakazi mmoja baada ya mwingine.Huyu ni Stela Alexanda

 Wakafuata wafanyakazi wengine pamoja na wakazi wa kata jirani na kiwanda yaani Sisitila na Ikuti

 Kama ilivyo kawaida katika kupima HIV kila mmoja katika foleni ya kuingia kwa mnasibu/mshauri nasaha alikuwa akijiuliza majibu yatakuwaje.Kijasho chembamba kikawa kinamtoka kila mmoja.

Baada ya kupima na kupokea majibu Meneja wa kiwanda akaona umuhimu wa kuzungumza na wawakilishi wa vyombo vya habari

 Mazungumzo ya Meneja yakamvuta mwakilishi wa kituo cha Luninga cha STAR TV Husna Mlanzi na kuamua kupima pia kama alivyoamua Hosea Cheyo wa TBC ambaye hayupo pichani.
 Hakupenda kwa wakati huo apokee simu yoyote ile.Akaamua kuizima simu yake kabisaaaa.
 Kupima si tatizo sana,kungoja majibu ndiyo kazi.Husna akaanza kuwaza damu tayari imechukuliwa je majibu yangu yatakuwaje?
Hamasa ya kupima ikamkuna mmiliki wa blogu ya Lyamba Lya Mfipa.Akaamua kuingia ulingoni.Ni baada ya kujiuliza iwapo watu wote wamepima ninachoogopa ninini.Na kama ni majibu si yatakuwa mali yangu bila kujalisha ni mazuri au mabaya.

 Swali la kujiuliza ni je wewe unasubiri nini kuijua afya yako?Tambua Tanzania bila maambukizi mapya inawezekana!Hongera TBL Mbeya
Shughuli ikafungwa rasmi ambapo zaidi ya watu 190 wamepima ikiwa ni mpango wa kiwanda cha bia cha TBL mkoani Mbeya kama maandalizi ya siku ya ukimwi duniani ambayo kimkoa yatafanyika desemba mosi wilayani Mbozi.

No comments:

Post a Comment