Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, May 6, 2014

MAFURIKO YASABABISHA HASARA YA BILIONI 2.3 KWA KUHARIBU BARABARA WILAYANI KYELA

MAFURIKO yaliyoikumba wilaya ya Kyela hivi karibuni yalisababisha hasara ya zaidi ya shilingi Bilioni 2.3 kutokana na uharibifu wa miundombinu ya barabara wilayani hapa. Mkuu wa wilaya ya Kyela Magreth Malenga amesema kiasi hicho cha fedha kinahitajika ili kurejesha miundombinu ya barabara za Halmashauri ya wilaya hiyo katika hali ya kawaida baada ya kuharibiwa vibaya na mafuriko. Malenga ameyasema hayo alipokuwa akitoa tathmini ya athari zilizotokana na mafuriko wakati akipokea msaada wa vitu mbali mbali kutoka Benki ya NMB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini msaada uliokuwa maalumu kwaajili ya waathirika wa mafuriko. Malenga amesema miundombinu ya barabara katika kuvifikia vijiji ni mibaya na haipitiki kabisa hali inayosababisha baadhi ya waathirika wa mafuriko kutofikiwa kwa wakati hivyo ili iweze kurudi katika hali yake ya kawaida zinahitajika kiasi hicho cha fedha kwa barabara za Halmashauri pekee.

No comments:

Post a Comment