Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Thursday, May 1, 2014

WAPONGEZA POLISI WA BARABARANI KUTIMULIWA KAZI

JESHI la polisi mkoani Mbeya limepongezwa kwa kuwachukulia hatua stahili askali wa jeshi hilo walioonekana kupotoka kimaadili na kulisababishia jeshi hilo aibu. Wakazi mkoani Mbeya wakiwemo madereva na makondakta wa gari za abiria wamelipongeza jeshi hilo na kulitaka liendelee na msimamo madhubuti wa kuwawajibisha askari wanaoonesha kupotoka kimaadili. Pongezi za wananchi kwa jeshi la polisi zinakuja kufuatia jeshi hilo kuwatimua kazi askari wake sita wa kikosi cha usalama barabarani baada ya kuridhishwa na viashiria vilivyoonesha askari hao kuhusika na masuala ya utovu wa nidhamu ikiwemo kupokea kushawishi na kupokea rushwa. Askari hao sita waliotimuliwa kazi ambao sasa watafikishwa mahakamani ni kutoka katika wilaya za Rungwe na Mbeya mjini ambao walibainika kufanya makosa hayo kwa nyakati na maeneo tofauti. Kamanda wa Polisi Mkoani hapa Ahmed Msangi aliwatataja askari waliotimuliwa kazi tangu Aprili 24 waliokuwa wakifanya kazi wilaya ya Mbeya mjini barabara ya Mbeya/Tunduma eneo la Songwe kuwa ni Copro Jonson,PC Rymond na PC Simon. Msangi aliwataja wengine kuwa ni Sajini Hezron,PC Shaban na PC Kajolo ambao walikuwa wakifanya kazi katika barabara ya Mbeya/Kyela maeneo ya wilaya ya Rungwe. Kamanda huyo alisema askari hao walikuwa wanakabiliwa na makosa hayo na walifunguliwa mashitaka ya kijeshi na hukumu kutolewa Aprili 24 mwaka huu na kupewa adhabu ya kufukuzwa kazi kabla ya kuwafikisha katika mahakama ya kawaida kujibu mashitaka yanayowakabili. Lakini baadhi ya wakazi wakiwemo madereva na makondakta wa gari za abiria walilitaka jeshi hilo kutoishia hapo badala yake lizidi kuwachunguza askari wake hususani wa kikosi cha usalama barabarani kutokana na baadhi yao kukithiri katika vitendo vya rushwa.

No comments:

Post a Comment