Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, May 20, 2014

CHATU MDOGO AKAMATWA,HOFU YATANDA ALIKO CHATU MKUBWA

Mganga wa Jadi Mazoea Hamisi(30) mkazi wa Chalinze mkoani Pwani(Kushoto) na msaidizi wake Athman Keneth(30) mkazi wa Chunya wakimwonesha chatu waliyemkamata HATIMAYE juhudi za kumsaka nyoka mkubwa aina ya Chatu anayesadikiwa kuwepo maeneo ya pembezoni mwa mto Meta jijini Mbeya zimeanza kuzaa matunda baada ya Chatu mdogo anayesadikiwa kuwa mtoto kukamatwa. Juhudi za kuanza kumsaka nyoka huyo zilianza siku chache baada ya mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Mbeya kutoa taarifa ya tahadhari kwa wakazi juu ya uwepo wa nyoka huyo mkubwa katika eneo hilo na kuwataka wakazi kuwa makini wanapopita katika njia za mkato zilizopo kwenye maeneo anayotajwa kuonekana. Hatimaye leo juhudi za kumsaka chatu huyo zilionekana kuanza kuzaa matunda baada ya wataalamu ambao ni waganga wa jadi wakishirikiana na maafisa maliasili kutoka halmashauri ya kiji kufanikiwa kumnasa chatu mdogo anayesadikiwa kuwa ni mtoto wa chatu ambaye amekuwa akionekana. Majira ya asubuhi leo wataalamu hao wakiongozwa na Mazoea Hamisi(30) mkazi wa Chalinze mkoani Pwani wameweza kumnasa chatu mdogo katika waliyemkuta pembezoni mwa Mto Meta jirani na hoteli ya Rift Valley. Siku ya kwanza wataalamu hao waliweza kumsaka nyoka huyo walini hawakuweza kufanikiwa zaidi ya kubaini njia ambazo amekuwa akipita na dalili zikaonesha kuwa alipita jana yake na si siku nyingi. Alisema jioni yake baada ya kupumzika waliona waweke dawa za kienyeji ambazo zingeweza kumtoa mafichoni na kusogea karibu ambapo asubuhi waliwahi kuendelea kumtafuta. Alisema baada ya muda kidogo wakati akiendelea kufyeka vichaka lakini kwa bahati nzuri alimkanyaga chatu huyo na yeye kukurupuka ndipo alipofanikiwa kumkamata. Kwa mujibu wa mganga huyo ambaye anasaidiwa na Athman Keneth(30) mkazi wa Chunya mkoani hapa, Chatu aliyekamatwa ni mdogo na juhudi za kuendelea kumtafuta mkubwa zitaendelea kama kweli yupo. Alisema mara nyingi Chatu mdogo anapoonekana Mkubwa anakuwa amehama ili kuwapisha wadogo kuendelea na maisha yao ama huyo mdogo alisombwa na maji kipindi cha mvua kutoka kwenye hifadhi na wenzie.

No comments:

Post a Comment