Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Friday, June 6, 2014

MBIO ZA MWENGE WA UHURU MKOANI MBEYA

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akiupokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Rukwa Eng.Stella Manyanya Hapa Kandoro akimpokea kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Rachel Kassanda baada ya kuwapokea wakimbiza mwenge wenzake watano kama unavyowaona hapo juu. Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari za Hollywood za wilayani Mbozi wakiushika mwenge wa Uhuru wakati mwenge huo ulipofika shuleni kwao.Mbele yao ni mmoja wa wakimbiza mwenge kitaifa Luteni Tanu Mlowezi Mmoja wa wakimbiza mwenge kitaifa Wito Mlemelwa akikagua moja ya mabwawa ya kufugia samaki wakati mwenge wa uhuru ulipotembelea eneo la kilimo mseto mali ya Molihan Mwamlima mkazi wilayani Mbozi. Mmoja wa wakimbiza mwenge wa uhuru kitaifa Yusuph Shesha akiweka bango lenye ujumbe wa onyo linalokataza wakazi kuingia na kufanya shughuli kinyume cha utaratibu katika hifadhi ya msitu wa asili wa Mapara uliopo wilayani Mbeya Mlemavu wa viungo Pendo Kwilukwa akiwa ameshika mwenge wa uhuru mara baada ya mwenge huo kukagua na kuweka jiwe la msingi katika jengo la zahanati ya kijiji cha Sinyanga wilayani Kyela iliyojengwa kwa jumla ya shilingi milioni 121 ambapo fedha kutoka serikali kuu ni shilingi milioni 83,wananchi shilingi milioni 30 na halmashauri ya wilaya ya Kyerla shilingi milioni nane Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa Rachel Kassanda akiteketeza pombe haramu aina ya viroba vinavyoingizwa wilayani Kyela kwa njia za panya zikitokea nchi jirani ya Malawi. Katibu tawala wa Mkoa wa Mbeya Marium Mtunguja akikabidhi mwenge wa uhuru kwa viongozi wa mkoa wa singida baada ya mwenge huo kukimbizwa katika wilaya nane na halmashauri 10 za mkoani Mbeya.

No comments:

Post a Comment