SIKU chache baada
ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk.Emmanuel Nchimbi kutangaza ongezeko la
vitendo vya uharifu ikiwemo mauaji ya kutumia silaha na kutoa onyo kwa
watanzania wanaomiliki silaha kiholela kuzisalimisha ndani ya siku 30 watu
wawili wanashikiliwa na polisi mkoani Mbeya kwa umiliki wa aina hiyo wa silaha.
Miongoni mwa
wanaoshikiliwa ambao wote walikamatwa na askari wanyamapori ni pamoja na
mwanamke Esther Msigwa(30) mkulima na mkazi wa Kijiji cha Madibira wilayani
Mbarali.
Kaimu kamanda wa
polisi mkoani hapa Adam Simfukwe amesema Esther amekamatwa Desemba 5 mwaka huu saa
saba mchana na askari wanyamapori waliokuwa doria na kwakuwa mtuhumiwa amekuwa
akijihusisha na uwindaji haramu ndipo waliamua kufanya msako nyumbani kwake na
kukuta bunduki moja aina ya Gobole aliyokuwa ameificha chumbani kwake.
Katika msako huo
pia askari hao wa TANAPA wamemkamata Badede Chafumbo(49) mkazi wa kijiji hicho
baada ya kukuta anamiliki gobore moja goroli 41 ambazo hutumika kama risasi na
chupa mbili za baruti.
Simfukwe amesema
silaha hizo zote zimekuwa zikitumiwa na mtuhumiwa kwa uwindaji haramu katika
hifadhi ya Ruaha iliyopo jirani na kijiji cha Madibira jambo ambalo ni kinyume
cha sheria.
No comments:
Post a Comment