Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, December 4, 2012

OFISI ya Katibu Tawala mkoani Rukwa imefikishwa katika mahakama kuu ya
kazi kanda ya nyanda za juu kusini iliyopo jijini Mbeya kwa kukiuka
makubaliano ya kumlipa mtumishi madai ya malipo ya uhamisho
yaliyowekwa chini ya Tume ya usuluhishi na maamuzi.

Mnamo Juni 7 mwaka huu tume hiyo ilisuluhisha mgogoro wa madai kati ya
Dereva Revocatus Nkonje na ofisi ya katibu tawala mkoa wa Rukwa kwa
makubaliano ya ofisi hiyo kumlipa mtumishi huyo kwa awamu jumla ya
shilingi 14,000,000.

Kiasi hicho cha fedha kilipunguzwa kutoka shilingi 60884,000 alizokuwa
akidai mtumishi ikiwa ni gharama za uhamisho baada ya mlalamikaji
kuridhia ombi la mdaiwa na ndipo makubaliano yakawa fedha hizo zilipwe
kwa awamu shilingi 2500,000 kila mwezi na muda wa ukomo ikapangwa iwe
desemba mwaka huu.

Kinyume na makubaliano yaliyofikiwa ofisi hiyo ilikaidi kwa kutomlipa
dereva huyo hali iliyopelekea kuchukua maamuzi ya kupeleka shitaka
hilo katika mahakama kuu ya Kazi iliyopo jijini Mbeya ili kuomba
kukazia hukumu.

Awali shitaka hilo ilikuwa lianze kusikilizwa novemba 28 mwaka huu
lakini limesogezwa mbele hadi desemba 3 mwaka huu.

Akizungumza na gazeti hili jijini Mbeya mara baada ya kuahirishwa kwa
shitaka lake Nkonje alisema baada ya kufikisha shitaka hilo mahakamani
hapo hali ya utumishi wake imekuwa katika misukosuko na manyanyaso
makubwa toka kwa mwajiri.

Alisema ni zaidi ya mwezi mmoja umepita tangu azuiliwe kuendesha gari
ya idara ya afya katika hospitali ya mkoa wa Rukwa aliyokuwa
akiendesha siku zote na pia amezuiwa kuendesha gari nyingine yoyote
bali kila siku afike ofisini kwake na kuripoti.

Alisema alipohoji sababu ya kuzuiwa aliambiwa ni kwakuwa amempeleka
katibu tawala katika mahakama kuu ya kazi hivyo jambo ambalo
halijampendeza na kuamua kutoa adhabu hiyo.

Kwa mujibu wa Nkonje madai yake ni ya uhamisho wa muda uliofanyika
Agosti 14 mwaka 2009 alipotolewa wilayani Mpanda kwenda ofisi za mkoa
wa Rukwa ambapo madai halisi yalikuwa shulingi 60884000 lakini mpaka
leo hajalipwa hata shilingi moja licha ya kukubali kupunguza madai
hayo hadi shilingi milioni 14.

No comments:

Post a Comment