Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, December 11, 2012

ASKARI MAGEREZA AUAWA NA MWILI KUCHOMWA MOTO

WATU wawili akiwemo Askari Magereza wa gereza la Luanda jijini Mbeya wameuawa kwa kupigwa na kuchomwa moto na wananchi wakidhaniwa kuwa wezi wa pikipiki. Askari aliyeuawa ametambulika kwa jina la Abel Mwakajinga(24) aliyekuwa likizo na nduguye Ezekiah Gambi(30)mkazi wa Chizumbi Wilayani Mbozi ambapo wameuawa walipokwenda katika kijiji cha Ukwile kata ya mlangali Wilaya ya hapa kwa lengo la kumkamata mtuhumiwa wa mauji ya ndugu yao. Mwenyekiti wa kijiji cha Ukwile Osiah Mtawa amesema tukio hilo limetokea Desemba 8, mwaka huu majira ya saa 10:00 jioni katika kijiji hicho ambapo marehemu hao wakiwa wanandugu walifika kijijini hapo kwa njia ya pikipiki ya kukodi(Bodaboda) wakilenga kumkamata Laiton Nganya anayetuhumiwa kwa mauaji ya ndugu yao Salum Gambi aliyeuawa Novemba 14, mwaka huu. Baada ya kufika katika kijiji hicho askari magereza alishuka na kwenda moja kwa moja kumkamata mtuhumiwa lakini kabla ya kutimiza malengo yake mtuhumiwa huyo alipiga yowe kuomba msaada wa wanakijiji akisema amevamiwa na wezi wa pikipiki na ndipo wananchi wakaanza kuwashambulia kwa kuwachoma na vitu vyenye ncha kali na hatimaye kuwachoma moto hadi kufa. Mdogo wa marehemu Ezekiah Gambi aliyejitambulisha kwa jina la Godfrey Gambi(26) amesema ndugu zake walikwenda katika kijiji hicho kwa lengo la kumkamata mtuhumiwa wa mauji ya ndugu yao baada ya kupata taarifa ya uwepo wake kijijini hapo lakini hakamatwi na polisi. Akizungumza kwa njia ya simu kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athuman alikiri kuwa na taarifa za tukio hilo na kusema tayari watuhumiwa wa mauaji hayo wametambuliwa na utaratibu unafanyika ili waweze kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

No comments:

Post a Comment