Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Thursday, December 6, 2012

WAHAMIAJI HARAMU

WAHAMIAJI haramu 28 wote raia wa Ethiopia wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Mbeya kwa kuingia nchini kinyume cha sheria.

Kadhalika jeshi hilo linamshikilia dreva taxi aliyefahamika kwa jina la Christopher Alfred(39) mkazi wa Veta jijini Mbeya kutokana na wahamiaji hao haramu kukutwa katika pagala la nyumba yake anayoendelea kuijenga.

Kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa Adam Simfukwe amesema kuwa wahabeshi hao wamekamatwa na askari waliokuwa doria desemba 5 mwaka huu majira ya saa  4:00 usiku katika eneo la Veta jijini Mbeya.

Simfukwe amesema watuhumiwa wakiongozwa na mwenzao aliyefahamika kwa jina la Mohamed Kabebe(27) walikuwa wamejificha ndani ya pagala hilo lakini haikufahamika mara moja waliingia jijini hapa wakitokea wapi na ni wapi wanakoelekea.

Amesema taratibu za kisheria zinaendelea kufanyika ikiwa ni pamoja na kuwakabidhi wahamiaji hao kwa Idara ya Uhamiaji ili iendelee na mchakato mwingine wa kisheria dhidi yao.

No comments:

Post a Comment