Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Wednesday, December 12, 2012

CHADEMA WAKANA KUMJUA EDO MWAMALALA

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) wilayani Mbeya kimekana kumtambua aliyewahi kuwa katibu wa chama hicho mkoa Edo Mwamalala kikisema kilikwishja mtimua miezi mitatu iliyopita hivyo matamko anayoyatoa kupitia vyeo anavyojipa si ya cha hicho. Uongozi wa chama hicho umeyasema hayo katika kikao chake na waandishi wa habari na kubainisha kuwa Mwaalala alikwisha timuliwa uanachama baada ya kamati tendaji ya chama wilaya kujiridhisha kuwa hakisaidii chama bali ni miongoni mwa watu wanaokisaliti. Hata hivyo kauli ya kutanganzwa kufutiwa uanachama imekuja baada ya Mwamalala kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini akithibitisha katibu mkuu wa Chadema dk.Wilbrod Slaa kuendelea kuwa na kadi mbili za vyama vya siasa ikiwemo ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) kauli ambayo imekuwa ikiwaumiza wanachadema kila inapotamkwa. Mwenyekiti wa Chadema Mbeya mjini David Mwambigija alisema jana kuwa japo ilikuwa haijatangazwa kwenye vyombo vya habari,Makata alienguliwa katika chama hicho muda mrefu kwa mujibu wa katiba ya chama hicho sura ya kumi kifungu cha tisa,kumi na kumi na moja. “Tulikwisha mfutia uanachama hivyo aliyetoa taarifa kwenye vyombo vya habari majuzi ni mhuni wa mtaani tu.si katibu wa chama wala mjumbe wa mkutano mkuu kama alivyojiita.Hayupo tena Chadema ndiyo maana kwa sasa utamuona jirani sana na Thomas Nyembo wa chama kipya cha NDC” “Tulimgundua hakuwa mtu mwema kwa chama chetu bali mamluki.Mwamalala aliwahi kukutwa yuko na aliyewahi kuwa mwenyekiti wa chadema Sambwee Shitambala baadae akahamia CCM wakiwa wanataka kwenda Dodoma kuonana na Nape bahati mbaya wakakutana na Sugu ndipo kwa aibu akaamua kuahirisha hiyo safari” alisema Mwambigija. Alilalamikia kauli ya dk.Slaa kutajwa kuwa na kadi ya CCM akisema hakuna katiba inayosema lazima mwanachama anapokihama chama flani arejeshe kadi kwa chama anachokihama au akikabidhi chama anachohamia japokuwa ni mtindo ambao Chadema wamekuwa wakiutumia siku zote kunyang’anya kadi za wanachama wanaohamia kutoka vyama vingine. Alimtaja Mwamalala sawa na mbwa anayebweka baada ya kutimuliwa kwenye lindo ambako walau alikuwa akisukuma maisha klwa kuokota mifupa ndiyo maana haishi kutapatapa. Alisema kwa mujibu wa katiba ya chama chao hairuhusiwi mwanachama wa kawaida kumjadili kiongozi wa ngazi ya kitaifa nje ya vikao vya chama na kufanya hivyo ni makosa na angekuwa ni mwanachama wangeweza kumwajibisha

No comments:

Post a Comment