Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Monday, September 14, 2015

TBL YAALIKA WAFANYABIASHARA KUNUFAIKA NA KIWANDA MBEYA

WAFANYABIASHARA mkoani Mbeya wamehimizwa kutumia fursa ya uwepo wa kiwanda cha bia cha TBL mkoani kwao kwa kujihusisha na biashara zenye mahusiano na kiwanda hicho ili waweze kunufaika na uwepo wake.



Miongoni mwa fursa zilizopo ni pamoja na kuanzisha viwanda kwaajili ya kusaga unga wa mahindi utumikao katika kutengenezea bia.

Meneja wa kiwanda cha TBL Mbeya Waziri Jemedari alitoa hamasa hiyo alipozungumza na wanahabari mkoani hapa kwenye shindano la kuonja na kutambua ladha ya bia lililofanyika kiwandani na kuwashirikisha wanahabari kutoka vyombo mbalimbali.



Jemedari alisema bado wafannya biashara na wakulima mkoani Mbeya hawajaitumia vyema fursa ya uwepo wa kiwanda hicho hatua inayopelekea wenzao kutoka maeneo ya mbali kunufaika na fursa hiyo.



Alisema licha ya mkoa wa Mbeya kuwa miongoni mwa mikoa inayozalisha kwa wingi mahindi,bado kiwanda hicho kinalazimika kuagiza unga kutoka Arusha,Iringa,Kibaigwa na Dar es salaam.



“Wafanyabiashara wa Mbeya bado wamejikita katika biashara nyingine ikiwemo ya kununua nafaka kutoka kwa wakulima na kuziuza tena pasipo kuziongezea thamani.Hii inatulazimu kuagiza unga wa mahindi wa dona kutoka mbali wakati hapa mahindi yanalimwa kwa wingi.”



“Nadhani hawajatambua uwepo wa kiwanda hiki unavyoweza kuwanufaisha.Hatuwezi kufungua viwanda vya kusaga unga wa dona kwakuwa tutakuwa tunawanytima wengine fursa.Sisi tunatengeneza bia,tunahitaji wadau wengine wa kutuzalishia malighafi za kulisha kiwanda chetu” alisisitiza.



Alisema kwa sasa mahitaji ya unga wa mahindi wa dona kiwandani hapo ni mkubwa ambapo jumla ya tani 30 hutumika kwa kila juma moja hivyo ni fursa nzuri kwa watakaopenda kuwekeza kwenye uzalishaji wa malighafi hiyo.



Alisema TBL iko tayari kukutana na mfanyabiashara yeyote atakayeonesha nia ya kuwekeza katika biashara hiyo na itahakikisha inampa mwongozo juu ya namna gani malighafi inayohitajika na kiwanda inavyopaswa kutengenezwa.



Aliitaja fursa ya kilimo cha Shayiri kuwa faida nyingine ambayo wakazi wa Mbeya hawajawekeza ipasavyo kwani hadi sasa kwa mkoani hapa ni wakulima wa wilaya ya Mbozi pekee wanaozalisha huku kiwanda kikilazimika kununua bidhaa hiyo kutoka maeneo mengine ikiwepo Sumbawanga mkoani Rukwa.



Alisema licha yak ampuni kutoa fursa ya kuwawezesha wakulima katika shughuli mbalimbali za uzalishaji wa zao hilo,bado mwitikio wa wakulima mkoani hapa ni mdogo mno katika kilimo cha zao la Shayiri wakati soko ni la uhakika.

Katika shindano la kuonja bia,mtangazaji wa Mbeya FM David Nyembe anayekabidhiwa katoni ya bia aina ya Kilimanjaro Twist pichani aliibuka mshindi akifuatiwa na mwakilishi wa ITV mkoani hapa Emmanuel Lengwa aliyeshika nafasi ya pili.


No comments:

Post a Comment