Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, March 13, 2012

zambi aunguruma uchaguzi wa kiwira


MBUNGE wa jimbo la Mbozi mashariki, Godfrey Zambi (CCM), amewataka wananchi wa kata ya Kiwira, wilayani Rungwe kutojaribu kufanya majaribio kwa kumchagua mgombea ambaye hana uwezo ili awaongoze.

Mbunge huyo amesema kufanya hivyo ni sawa na kuyaweka rehani maendeleo ya kata hiyo kwa kipindi kirefu kijacho, hali ambayo itawafanya wajutie uamuzi wao huo iwapo hawatakuwa makini.

Zambi ametoa rai hiyo jana wakati akizindua rasmi kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Kiwira wilayani Rungwe, uliofanyika viwanja vya soko la Tandale, Kiwira.

Amefafanua kuwasema mmoja wa wagombea aliyejitokeza ni mwanafunzi, hivyo ni vyema wananchi wamnyime kura ili aende akamalize kwanza masomo yake, ili baadaye ndipo aombe uongozi na siyo sasa. 

Kwa hisani ya mtandao

No comments:

Post a Comment