Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Monday, March 5, 2012

MCHUNGAJI ALIYEKAMATWA NA VIUNGO VYA BINADAMU AHUKUMIWA MIAKA NANE JELA


MCHUNGAJI wa kanisa la Assemblis Of  God KOSIMAS  MWASENGA na mwenzake LUSEKELO MWASHILINDI wamehukumiwa kifungo cha miaka nane jela kila mmoja kwa kosa la kukutwa na viungo vya binadamu.

Hakimu mfawidhi wa mahakama ya mkoa Monica Ndyekobora amesema washitakiwa walikuwa wanakabiliwa na mashitaka matatu nayo ni kukutwa na viungo vya binadamu, kula njama ya kuuza viungo vya binadamu na kukutwa na madawa aina ya PPF chupa 18 za dawa na chupa 14 za maji.

Awali akisoma mashtaka yanayowakabili washitakiwa hao wawili mwanasheria wa Serikali Christine Joas amesema watuhumiwa walikamatwa Februari 13 mwaka 2009 maeneo ya Mlowo wilayani Mbozi wakiwa na viungo vya binadamu vilivyokuwa vimefichwa bafuni.

No comments:

Post a Comment