Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Thursday, March 15, 2012

MULUGO AZIKOROMEA SHULE ZA NYANDA ZA JUU KUSINI

NAIBU waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Filipo Mlugo (CCM) ametoa onyo kwa baadhi ya wakuu wa shule za sekondari za nyanda ya juu kusini kuacha udanganyifu wa mitihani ya wanafunzi wa ngazi zote.

Akizungumza katika warsha ya kujengeana uwezo kwa wamiliki ,mameneja,wakuu wa shule ,na vyuo visivyo vya serikali alipoitwa kuwa mgeni  rasmi na cham cha Tanzania Association of managers and owners of non-government ilyofanyika maeneo ya Catholic Youth Centre mkoani hapa hivi karibuni.

Mlugo alisema idadi kubwa ya wakuu wa shule za sekondari siyo waaminifu katika mitihani ya wanafunzi kwani wengi wao wamekuwa wakijaza ripoti za uongo zinazotakiwa kufikshwa makao makuu kwa lengo la kuangalia matokeo ya awali ya wanafunzi hao .

Aidha aliongeza kuwa sababu inayopelekea udanganyifu wa mitihani kwa upande wa shule zisizo za kiserikali ni uzembe pamoja na uvivu wa mameneja wa shule hizo kwa kutokuwa karibu na walimu wakuu waliyowaajiri katika shule zao kwani wangekuwa karibu kwa kuwafuatilia walimu ingekuwa rahisi kuwagundua wanaofanya uharifu huo na ikiwezekana kuwaondoa madarakani na vidhibitisho kamili.

"Utakuta mwanafunzi katika matokeo ya mitihani ya utamilifu (MOCK)
                        yanaonyesha amefaulu sana kuanzia alama 90-100 kwa baadhi ya masomo wakati huo huo katika mitihani ya mwisho matokeo yanaonyesha amefeli kabisa kwa masomo yale yale yaani anakuwa na ziro kila somo na kuandika nyimbo za bongo fleva ,je mitihani ya nyuma aliwezaje kufaulu ."Alihoji Mulugo.

                        Vile vile Mlugo aliwataka mameneja wote kwaajibisha walimu wanaobaika wakifanya udanganyifu wa mitihani ili kuepuka adhabu ya kufungiwa shule endapo wataonekana kuwa na makosa ya udanganyifu na kuwa wamiliki wa shule hizo wajue wao wapo kwa niaba ya serikali hivyo wawe makini kwa kusimamia shule zote ili kusaidiana na serikali .

"Natoa onyo kuwa mkuu wa shule yeyote atakayebainika amefanya udanganyifu wa mitihani ya taifa hasa darasa la saba,kidato cha nne,kidato cha sita na vyuoni atapewa adhabu kali " Alisema
                         .
Aliongeza kuwa baadhi ya benki zimekuwa na udanganyifu pindi wanafunzi wa vyuo vikuu wanapotumiwa fedha za mikopo na serikali haziwafikii wanafunzi kwa muda  muafaka na hivyo kupelekea maandamano na migomo kwa lengo la kudai haki zao .

Kadhalika naibu waziri huyo aliisifu shule ya St;Francis iliyopo jijini Mbeya kuwa imekuwa ikitupatia sifa ya kitaifa kila mwaka kwa  matokeo mazuri ya kidato cha nne na aliwasihi wajenge madarsa mengine ya kidato cha tano na cha sita .

Mlugo alisema mitihani ya kidato cha pili itaendelea kuwepo na atakayefeli atalazimika kurudia kidato hicho baada ya kubaini kuwa wanafunzi wanaohitimu kidato cha nne wanafeli sana .

No comments:

Post a Comment