Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Wednesday, March 28, 2012

CHADEMA YAMWAIBISHA MEYA MBEYA

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimeongoza katika uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa uliofanyika Mbeya mjini jumapili iliyopita kwa kupata wajumbe wa mitaa 29 kati ya mitaa 47 iliyofanya uchaguzi huo.
Chama cha demokrasia na Maendeleo Chadema kilichokuwa chama pekee cha upinzani katika uchaguzi huo kilipata wajumbe 16 wa mitaa na mingi kati ya mitaa hiyo ikiwa ni ile iliyopo katika kata ya Itiji anakotokea meya wa jiji la Mbeya Athanas Kapunga.

Katika nafasi ya mwenyekiti wa mtaa wa Itiji anakotokea meya huyo ambaye pia ndiye katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM Mbeya mjini Chadema iliigalagaza CCM.

Msimamizi wa uchaguzi huo mkurugenzi mtendaji wa Juma Iddy akitangaza matokeo alisema katika kura 603za kumchagua mwenyekiti wa mtaa mgombea kupitia Chadema Ezekiel Kinga alipata kura 325 na wa CCM Athuman Chiba akapata kura 246 na kura 32 ziliharibika.

Kwa mujibu wa Iddy mgombea Kinga ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa mtaa huo awali lakini kutokana na tofauti kati yake na meya ikafikia hatua ya yeye kuvuliwa uanachama na ndipo nafasi hiyo ikabaki wazi.

“Kwa matokeo hayo mgombea kupitia Chadema ameshinda kuwa mwenyekiti wa mtaa wa Itiji.Kwa upande wa nafasi za wajumbe wa mitaa,kulikuwa na nafasi 47 za kujazwa katika mitaa 37” alisema.

Hata hivyo msimamizi huo alisema uchaguzi huo kwa nafasi za wajumbe utapaswa kurudiwa katika mitaa miwili kutokana na matokeo ya kura za wagombea zilizopigwa kugongana.

No comments:

Post a Comment