Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa ajari hiyo machi 19 mwaka huu,majira ya 2;30katika eneo la Senjele wilayani Mbozi mkoani Mbeya.
Kamanda Nyombi alisema ajari hiyo imehusisha gari yenye namba za usajiri T482 BQV aina ya Tyng mali ya kampuni ya Prince muro ambayo ilikuwa ikiendeshwa na dereva ambaye hakufahamika jina.
Alimtaja marehemu kuwa ni Deusdedit Joseph na kati ya waliojeruhiwa wapo wanawake 4 na wanaume 10 ambapo wote wamelazwa katika hospitali teule ya Ifisi iliyopo katika halmashauli ya wilaya ya Mbeya kwa matibabu.
Amesema kuwa uchunguzi zaidi juu ya chanzo cha ajali pamoja na juhudi za kumsaka dereva zinaendelea.
Baadhi ya mabaki ya vitu baada ya ajali hiyo jana usiku
Hili Ndilo Gari la mizigo ambalo basi la Prince Muro lilitaka kulipita, na baadae kushindwa na kupinduka baada ya kukutana na Gari lengine mbele yake
Shimo hili limechimbika wakati wa ajali hiyo ilipo tokea jana usiku
Hapa ndipo Basi la Prince Muro lilipo taka kuingia na kulikwepa gari hili na kupindukia upande wa pili
Muonekano wa gari hili la mizigo ambalo limeharibikia bara barani
Mmoja wa majeruhi ambae alikuwa anatokea Dar es salaam kwenda kuwasalimu ndugu zake Ileje aliye fahamika kwa jina moja tuu la Andendekisye akiwa katika Hospital ya Ifisi Mbeya Muda huu
Baadhi ya Majeruhi walio nusurika katika ajali hiyo wakiwa katika Hospitali ya Ifisi kuelekea katika matibabu na kutazamwa kama wamepata matatizo yoyote.
Hawa ni majeruhi kati ya wale 14
Mganga mkuu wa Hospitali ya Ifisi Dkt. Mbilinyi akiongea na moja ya majeruhi mapema leo.
Majeruhi ambao wamenusurika katika ajali hiyo mbaya wamesema kwamba dereva huyo alikuwa mwendo kasi tangia walipo fika mikumi, Wameendelea kudai kwamba walimpa onyo mala kadhaa lakini hakuweza kuwasikiliza na akaongeza mwendo kasi zaidi mpaka walipo pata ajali hiyo maeneo ya Senjele kuelekea Tunduma.
Mtu mmoja amefariki na wengine 14 wakmejeruhiwa wakiwemo wanawake wanne na wanaume 10
Mtu mmoja amefariki na wengine 14 wakmejeruhiwa wakiwemo wanawake wanne na wanaume 10
PICHA KWA HISANI YA MTANDAO WA MBEYA YETU
No comments:
Post a Comment