Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Thursday, March 22, 2012

ALIYEUPIGA MAWE MSAFARA WA WAZIRI NAHODHA APANDISHWA KIZIMBANI

 
Waziri wa Mambo ya ndani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Shamsi Vuai Nahodha, akizungumza na vyombo vya habari Jijini Dar es salaam. 
*****
Mkazi wa Kijiji cha Nelo Kiloleni mji mdogo wa Tunduma Mkoani Mbeya, Aludo Juma Sanga (28) leo amefikishwa mahakama ya Wilaya ya Mbozi mbele ya Hakimu mfawidhi mwandamizi, kwa kosa la kutishia na kumdhuru Waziri wa mambo ya ndani Mheshimiwa Shamsi Vuai Nahodha.

Mwendesha mashtaka Bwana John Mazwile ameiambia mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo wakati Waziri Nahodha akiwa ndani ya gari yenye namba WMN alipokuwa katika ziara,  Februari 3 mwaka huu, majira ya saa 3 na dakika 50 asubuhi maeneo ya Mwangaza Hotel Tunduma.
 
Habari na Ezekiel Kamanga

No comments:

Post a Comment