Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Monday, March 5, 2012

WAWILI WAUAWA KINYAMA MBEYA


WATU wawili wameuawa kikatili jijini Mbeya katika matukio `tofauti yaliyotokea machi 4 mwaka huu likiwemo la mmoja aliyepigwa hadi kufa na wananchi wanaodaiwa kuwa na hasira kali baada ya kukutwa akiiba nyanya shambani.

Marehemu katika tukio hilo ni mkazi wa kitongoji cha Uyole jijini hapa aliyetambulika kwa jina la Emmanuel Wilison(23-27) na kabla ya kifo chake alikutwa akiiba nyanya shambani kwa mkazi mwenzake Jacob Wilison(41).

Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Advocate Nyombi amesema tukio hilo limetokea majira ya saa 2 asubuhi na kubainisha kuwa mwenye shamba bwana Wilson anashikiliwa kwa mahojiano zaidi kuhusiana na mauaji hayo.

Tukio la pili ni la mkazi wa eneo la Airpot jijini hapa Shobi Polandi(54) aliyeuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiofahamika huku chanzo cha mauaji hayo kikiwa bado hakijulikani.

Kwa mujibu wa kamanda Nyombi mauaji ya Polandi yametokea saa 1.15 usiku katika kitongoji cha Isengo eneo la Airpot  na inasadikiwa kuwa alivamiwa na kuuawa na watu hao wakati akirudi nyumbani kwake na mwili wake umekutwa na majeraha makubwa matatu.

No comments:

Post a Comment