Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, March 27, 2012

MWINGINE KATI YA WATUHUMIWA WA MAUAJI WALIOTOROKA AKAMATWA

MTUHUMIWA mmoja kati ya wale watatu wa mauaji walioshirikiana na mtuhumiwa wa wizi kuvunja chumba cha mahabusu ya kituo cha polisi kati jijini Mbeya na kutoroka amekamatwa.
Kamanda wa polisi mkoani hapa Advocate Nyombi amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na kusema wenzake wawili bado hawajapatikanaa na jeshi hilo linaendelea na msako.
Amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Maneno Wiwa Kalinga ambapo yeye na wenzake wawili wanakabiliwa na tuhuma za mauaji lakini hivi karibuni wakiwa katika chumba kimoja cha mahabusu walitoboa ukuta na kutoroka pamoja na mahabusu mwenzao Fadhili Mwaiteleke(27) aliyekuwa anakabiliwa na tuhuma za wizi wa betri tatu za gari aliyekamatwa muda mfupi baada ya kutoroka.
Kamanda Nyombi amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa jana saa 10:00 alfajiri katika kijiji cha Ruanda Wilayani Mbozi na kikosi kazi cha askari wanaoendelea na msako wa kuwasaka watuhumiwa wengine wawili waliobaki.
Mahabusu hao walichimba ukuta wa chumba walimokuwa mnamo machi 22 mwaka huu usiku kati ya saa 8 hadi saa 9 huku askari waliokuwa zamu katika kituo hicho wakiwa hawajui lolote.

Kamanda Nyombi amesema mahabusu hao walitumia mbinu ya kulowanisha ukuta uliojengwa kwa tofali za saruji kuulainisha na baadaye wakatumia vipande vya nondo kuutoboa na kutoroka.

No comments:

Post a Comment