Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, July 15, 2014

AMAWAWA WAJENGEWA UWEZO NAMNA YA KUENDESHA ASASI YAO

.DIWANI WA KATA YA CHANJI MANISPAA YA SUMBAWANGA FELLICIAN MAVAZI AKIZUNGUMZA JAMBO WAKATI WA KUFUNGUA SEMINA Wawezeshaji Frank Msuku na James Kapele wakijadiliana jambo kabla ya kuanza kazi .Mwanasheria James Kapele akiendelea kufundisha juu ya Katiba ya asasi ya AMAWAWA .Mtaalamu wa masuala ya Fedha Frank Msuku akifafanua jambo alipokuwa akiwafundisha wajumbe wa bodi na wanachama wa AMAWAWA namna nzuri ya utunzaji wa mahesabu ya mapato na matumizi ya asasi yao CHANGAMOTO imetolewa kwa wadau wa kilimo wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa kujikita katika utoaji elimu ya kilimo kitakachowasaidia wakulima wilayani hapa kupiga hatua kimaendeleo. Diwani wa kata ya Chanji Manispaa ya Sumbawanga Fellician Mavazi alitoa changamoto hiyo alipokuwa akifungua semina ya siku moja ya kuwajengea uwezo wajumbe wa bodi na wanachama wa Asasi ya Maendeleo ya Wakulima na Wafugaji(AMAWAWA) ya wilayani hapa. Mavazi aliitaja Amawawa kuwa miongoni mwa wadau wanaopaswa kutoa mchango mkubwa kuhakikisha wakulima wanaachana na kilimo cha mazoea kisicho na tija na kugeukia kilimo cha kisasa. Alisema bado wakulima weengi wilayani hapa wanaendelea na kilimo cha kisasa ambacho kwa muda mrefu hakijawaletea faida licha ya kuwa wamekuwa wakitumia rasilimali nyingi. Hata hivyo alisema uelewa mdogo ndiyo chanzo cha wakulima kuendelea na kilimo cha asili lakini wachache wanaopewa elimu wamekuwa wakibadili mifumo ya kilimo chao na kujikuta wakipata mafanikio tofauti na awali. Katika semina hiyo iliyoandaliwa kwa hisani ya shirika la The Foundation For Civil Society,diwani Mavazi alilalamikia uwepo wa wawekezaji wanaohodhi maeneo makubwa ya ardhi kwa madai ya kuendesha kilimo cha kisasa lakini badala yake wanayatumia maeneo hayo kwa shughuli nyingine ikiwemo kukodisha mashamba kwa wakulima wadogo wadogo. Alisema wadau pia wanalo jukumu la kuhakikisha wanapigania hali hiyo na ikiwezekana ardhi ya wawekezaji wanaoshindwa kutekeleza masharti ya mikataba yao igawanywe kwa wananchi wa kawaida. Awali mwenyekiti wa Amawawa Oscar Msangi alisema malengo ya asasi hiyo ni kuhakikisha inatoa elimu ya kilimo cha kisasa kwa wakulima ili kuwezesha kilimo kuwa sehemu kubwa ya ajira nay a kutegemewa na vijana. Msangi alisema kwa vijana kujikita katika kilimo cha kisasa kitakachowapa manufaa zaidi ya kile cha sasa itapunguza wimbi la vijana kukimbilia mijini wakiamini ndiko kuliko na ajira nyingi na kujikuta wakiishia kujiunga na vikundi hatari.

No comments:

Post a Comment