Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Saturday, July 19, 2014

TAG YATOA PIKIPIKI KWA WACHUNGAJI WAANGALIZI

Wachungaji wa waangalizi wa kanisa la Tanzania Assemblies of God jimbo la kusini Magharibu wakiungana na waumini wa kanisa hilo kuombea pikipiki 15 zilizotolewa na kanisa hilo kwa wachungaji hao ili kusaidia utendajikazi wao. KANISA la Tanzania Assemblies Of Gog(TAG) limegawa pikipiki kwa wachungaji waangalizi 15 waliopo katika jimbo la kusini Magharibi. Akikabidhi pikipiki hizo jijini Mbeya,Makamu wa Askofu mkuu wa TAG Magnus Mhiche alisema lengo ni kuwezesha wachungaji hao kutekeleza majukumu kwa urahisi zaidi. Alisema kanisa lilianza mchakato wa kuboresha utendaji kazi kwa kununua na kugawa gari katika majimbo yote 32 sambamba na idara zote kumi za kitaifa za kanisa. Aliwataka wachungaji waliokabidhiwa pikipiki kuzitunza na kuhakikisha wanazitumia kwa shughuli za zilizolengwa badala ya kuanza kuzitumia kwa kusafirishia abiria. “Msije mkazigeuza boda boda,mkaona leo sina pesa ya mafuta basi mkawapa vijana jioni wazitumie kusafirisha abiria.Zitumieni kueneza neon la mungu” “Tumewapa usafiri ili mfike maeneo korofi yasiyofikika kwa gari.Lisaidieni kanisa kutimiza mkakati wake wa miaka kumi ya kuhubiri neon la Mungu.” Alisisitiza Makamu huyo wa askofu mkuu alisema fedha zilizotumika kununulia pikipiki hizo zimetokana na sadaka na michango mbalimbali ya waumini ambapo hadi kufikishwa jijini Mbeya kila pikipiki imegharimu kiasi cha shilingi milioni 3.6. Alisema mpango wa ugawaji pikipiki kwa wachungaji wangalizi utaendelea katika majimbo yote nchini lakini akasema zoezi hilo litafanyika kwa awamu tofauti. Kwa upande wao wachungaji waangalizi waliopewa walipongeza hatua ya uongozi wa kanisa kuwapa usafiri japo wa aina hiyo wakisema wamekuwa wakipata wakati mgumu kiusafiri wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku. Wachungaji Moses Kaminyoge wa seksheni ya Mlowo na mwenzake Paul Mfwomi wa Seksheni ya Tunduma walisema wakati mwingine wamekuwa wakiingia gharama kubwa kukodi vyombo vya usafiri ili kuyafikia maeneo ya mbali kutoa huduma.

No comments:

Post a Comment