Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Wednesday, July 2, 2014

LITA 400 ZA DAMU KUKUSANYWA KUTOKA KWA WACHUNGAJI WA KANISA LA TAG

. Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akipokea msaada wa vyandarua kutoka kwa Askofu mkuu wa kanisa la TAG Dk.Barnabas Mtokambali wakati wa uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa vyandarua.Jumla ya vyandarua 8,550 vitagawanywa na kanisa hilo kwa hospitali na vituo vya afya vilivyopo katika mikoa ya Mbeya,Rukwa na Njombe ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya sherehe za Jubilei ya miaka 75 ya kanisa hilo nchini Askofu mkuu wa kanisa la TAG Dk.Barnabas Mtokambali akizungumza jambo kabla ya kuzindua zoezi la ugawaji vyandarua. Baadhi ya watumishi wa hospitali ya Rufaa Mbeya na viongozi wa kanisa la TAG wakishuhudia uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa vyandarua JUMLA ya lita 400 za damu zinatarajiwa kukusanywa na benki ya damu kanda ya nyanda za juu kusini kutoka kwa wachungaji 800 wanaounda baraza la waangalizi la kanisa la Tanzania Asemblies of God(TAG). Wachungaji hao watachangia damu kwa hiari Julai 10 mwaka huu ikiwa ni sehemu ya mchango wao wa kijamii katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya jubilee ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo nchini yatakayofanyika Julai 13 mwaka huu. Askofu mkuu wa wa kanisa la TAG Barnabas Mtokambali ametoa ahadi hiyo wakati wa uzinduzi wa huduma ya kijamii ya utoaji wa vyandarua 8,550 vitakavyogawaiwa katika mikoa ya Mbeya,Rukwa na Njombe. Askofu Mtokambali amesema zoezi la uchangiaji damu litafanyika katika Chuo cha Biblia cha TAG kilichopo maeneo ya Itende jijini Mbeya na kubainisha kuwa taratibu zote za mawasiliano na ofisi ya kanda ya Damu salama zimekamilika. Hata hivyo askofu huyo amesema iwapo itabainika kuwepo na uhitaji zaidi wa damu hamasa itafanyika kwa wageni wengine mbalimbali wapatao takribani 600 ili nao waweze kuchangia damu kwa hiari kabla ya siku ya kilele cha maadhimisho ya jubilee. Akitoa shukrani za serikali kwa ahadi hiyo sambamba na kupokea vyandarua 4,150 kwaajili ya mkoa wa Mbeya,mkuu wa mkoa huo Abbas Kandoro ameupongeza uongozi wa kanisa hilo kwa kuonesha moyo wa kuwajali wagonjwa pasipo kujali utofauti wa dini wala madhehebu.

No comments:

Post a Comment