Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Monday, September 15, 2014

KIMENUKA MBEYA CITY,WACHARAZWA GOLI 4-1 NA VIPERS FC YA UGANDA

 KIKOSI CHA MBEYA CITY
KIKOSI CHA VIPERS KUTOKA UGANDA

Ni kama vile hawakuwa katika uwanja wa nyumbani,Mbeya City mwishoni mwa wiki walijikuta wanatoka uwanjani wakiwa wameinamisha vichwa vya o kwa aibu mbele ya mashabiki baada ya kuambulia kipigo cha mbwa mwizi cha goli 4-1 kutoka kwa Vipers ya nchini Uganda.

Mchezo huo wa kirafiki umezua gumzo katika viunga vya jiji la Mbeya na maeneo ya jirani juu ya uwezo wa timu hiyo katika msimuu huu wa ligi kuu ya Tanzania bara.Wapo wanaohoji kuondoka kwa aliyekuwa kocha msaidizi wa timu hiyo ambaye inasemekana kutokana na migongano ya ndani ya uongozi wa timu hiyo aliamua kubwaga manyanga na kutafuta ustaarabu mwingine.Wapo pia wanaohoji je Mbeya City itaonesha makali yake ya msimu uliopita baada ya kuondoka kwa kocha huyo?

No comments:

Post a Comment