Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akiongeza jambo kwenye kikao hicho akikanya wanaopotosha umma kuwa kujiunga na CHF ni kujiunga na mtandao wa Freemasons
Baadhi ya madiwani wakifuatilia maelekezo ya mkuu wa mkoa
Wataaalamu wa halmashauri ya wilaya ya Kyela nao hawakuwa nyuma kufuatilia
MKUU wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro
amekemea vikali watu wote wanaopotosha umuhimu wa mfuko wa Afya ya Jamii(CHF)
wakisema ni njia ya kuwaingia wananchi katika mtandao wa Freemasons.
Kwa wilayani Kyela,kupitia CHF kila
mkazi anapaswa kulipia kiasi cha shilingi 5000 ili aweze kupata huduma za afya
bure kwa kipindi cha mwaka mzima.
Lakini tafsiri ya bima hiyo kwa
baadhi ya wakazi wilayani humo imekuwa ni kuhusisha upatikanaji wa huduma
kupitia CHF na mtandao wa Freemasons wakisema haiwezekani watu wakapata tiba
kwa kiasi kidogo cha fedha kama shilingi 5000 kwa mwaka mzima.
Akiwa katika kikao cha baraza maalumu la madiwani kilichokuwa kwaajili ya kupitia na kujadili taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali(CAG) kwa mwaka wa fedha 2012/2013 Kandoro amekemea vikali upotoshaji huo.
Amesema iwapo wapo watu ambao
hawahitaji kaya zao kujiunga na mfuko wa CHF basi wanapaswa wakae kimya na
kuendelea kugharamia matibabu yao badala ya kuendeleza uvumi na kuipotosha
jamii na kuisababishia kuami katika mambo yasiyo na msingi kwao.
Mkuu huyo wa mkoa pia ameagiza
uongozi wa wilaya kuhakikisha unatoa maagizo kwa viongozi wa vijiji na kata
kuendelea kutoa hamasa kwa jamii kujiunga na mfuko huo ili kupunguza gharama za
matibabu.
Aidha ametaka pia kuchukuliwa kwa
hatua za kisheria kwa mtu yeyote atakaeendeleza maneno ya upotoshaji akihusisha
huduma zitolewazo na CHF na mtandao wa Freemasons kwakuwa mtu huyo atakuwa
haitakii mema jamii inayomzunguka.
No comments:
Post a Comment