Afisa mradi wa GBV na VAC kupitia kanisa la Anglikana akiwasilisha taarifa za utendaji kazi wa mradi huo unaoendeshwa katika kata za Ilembo na Masoko wilayani Mbeya kwa hisani ya watu wa marekani.
Baadhi ya wajumbe wa kamati za Maendeleo za kata za Ilembo na Masoko,wakifuatilia kwa makifuatilia kwa makini taarifa ya utekelezaji wa mradi wa GBV na VAC ilipokuwa ikiwasilishwa Afisa wa mradi huo kwenye kikao cha tathmini ya mradi.
Mmmoja wa waelimishaji wa mradi wa GBV na VAC getrude Elisha akibainisha namna waelimishaji wa mradi huo wanavyotishiwa maisha na watuhumiwa wa vitendo vya ukatili katika vijiji wanavyofanyia kazi ndani ya kata za Ilembo na Masoko wilayani Mbeya.
Muelimishaji Eslom Nsyesye akibainisha changamoto wanazokumbana wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ndani ya kata hizo mbili.
HABARI KAMILI.....
WAELIMISHAJI wa masuala ya kupinga ukatili wa
kijinsia(GBV) na ukatili dhidi ya watoto(VAC) katika kata za Masoko na Ilembo
wilayani Mbeya wamedai kutishiwa maisha yao na watuhumiwa wa matukio ya
ukatili.
Katika kikao kikao kilichofanyika jana kijijini
Masoko wilayani hapa,waelimishaji hao kupitia mradi wa GBV unaoendeshwa na
kanisa la Anglikana kwa hisani ya watu wa Marekani walisema wana wakati mgumu
hivi sasa kwani kutoa kwao elimu kumegeuka shubiri kwao.
Mmoja wa waelimishaji hao Getrude Elisha alisema
wamekuwa wakipokea vitisho vingi kutoka kwa watuhumiwa wa vitendo vya ukatili
wakiwaonya kutoendelea na tabia ya kuwapa ufahami juu ya hatua gani wachukue
watu waliotendewa ukatili.
Getrude alisema hivi sasa waelimishaji hao
wanashindwa kutembea wakiwa peke yao hususani nyakati za usiku kwakuwa wanahofu
wanaweza kuvamiwa na kujeruhiwa kama si kuuawa na watu wanaowatishia kila
kukicha.
“Msaada wetu umegeuka tatizo kubwa kwetu.Tunatishiwa
maisha na watuhumiwa wa vitendo vya ukatili.Kwa sasa tunaogopa kutembea.Giza
likianza inabidi tuwe tumejifungia majumbani mwetu” alisema Getrude.
Muelimishaji mwingine Eslom Msyesye alisema hofu
zaidi kwa waelimishaji inatokana na viongozi waliopewa majukumu ya kulinda
amani wakiwemo maafisa watendaji kutowajibika kwa taarifa za matukio ya ukatili
wanazopelekewa.
Msyesye alisema waelimishaji wamekuwa wakitekeleza
wajibu wao wa kuwapa uelewa watu wanaofanyiwa ukatili lakini bara waathirika
wanapochukua hatua ya kutoa taarifa kwa maafisa watendaji taarifa hizo zimekuwa
zikiishia katika ofisi za viongozi hao kwa watendaji husika kupewa rushwa na
watuhumiwa.
Alisema matokeo ya upokeaji huo wa rushwa imekuwa ni
watuhumiwa kuendelea kurandaranda mitaani huku wakijitapa kuwa hakuna hatua
zozote zinazoweza kuchukuliwa na kuwanyooshea vidole waliotoa elimu kwa
muathirika kuchukua hatua.
Kwa upande wake afisa mradi wa GBV Patrick Kosima
alikiri kuwepo na taarifa za waelimishaji kutishiwa maisha na watuhumiwa wa
vitendo vya ukatili na kuahidi kupeleka suala hilo katika uongozi wa juu wa
wilaya ili kulinda usalama wao
Kosima pia aliwatupia lawama maafisa watendaji wa
vijiji na kata akisema wanachangia kuendelea kushamiri kwa vitendo vya ukatili
katika jamii wanazoziongoza kwakuwa hawachukui hatua stahili kwa watuhumiwa.
No comments:
Post a Comment