MFUKO wa Mafao ya Kustaafu(GEPF) umetajwa kukua kwa kasi katika
kipindi cha miaka 10 iliyopita na kuwezesha kuzidi kuongeza matawi nchini ili
kuwafikia wateja wengi zaidi.
Tayari GEPF imefungua tawi lake mkoani Mbeya na litakuwa likitoa
huduma za mafao yake kwa wateja walioko katika mikoa ya kanda ya nyanda za juu
kusini.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ofisi za
mkoani Mbeya zilizopo eneo la uhindini,Meneja Masoko wa GEPF Aloyce
Ntukamanzina alisema wanachama wa mfuko huo wameongezeka kutoka 16,131 mwaka
2004 na kufikia 76,000 mwaka 2014.
Ntukamanzina amesema mwaka 2004 mfuko huo uliweza kukusanya shilingi
bilioni 5.1,lakini mwaka huu umeweza kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 37.29.
Meneja Masoko huyo amesema mafanikio hayo yanatokana na sababu
mbalimbali ikiwemo uongozi bora na uwekezaji makini sambamba na mabadiliko ya
mfumo wa kiutendaji.
Amesema ujio wa GEPF ni fursa nyingine kwa wakazi wa mkoa wa
Mbeya,ya kujiwekea hazina ya mafao ya uzeeni ili watakapokuwa na umri
usiwawezesha kufanya shughuli za uzalishaji mali waweze kuendelea kuishi maisha
bora kama hapo awali.
Amesema bado kuna changamoto ya watanzania wengi kutopenda kujiunga
na mifuko ya hifadhi za jamii jambo alilosema limekuwa likisababisha watu wengi
kuishi maisha magumu mara wanapozeeka na kukosa nguvu za kufanya kazi za
uzalishaji mali.
No comments:
Post a Comment