KIKOSI CHA TANZANIA PRISONS
WAMILIKI wa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya
wameendelea na jitihada za kuukarabati uwanja huo ikiwa ni sehemu ya maandalizi
ya michuano ya ligi kuu ya Tanzania bara itakayoanza kutimua vumbi Septemba 20
mwaka huu.
Ukarabati unaoendelea hivi sasa katika uwanja huo
utakaotumiwa na Timu za Mbeya City na Tanzania Prison kama uwanja wa nyumbani
ni pamoja na kuondoa magugu yasiyohitajika katika eneo la kuchezea maarufu kama
Pichi.
Akizungumza na Lyamba Lya Mfipa,Meneja wa
Uwanja huo Modestus Mwaluka amebainisha namna shughuli nzima ya kuondoa magugu
hayo inavyoendeshwa,shughuli ambayo pia imesababisha Timu za Mbeya City na
Tanzania Prison kuzuiwa kuendelea kuutumia uwanja huo kwa mazoezi.
Mwaluka amesema wanalazimika kuyaondoa magugu hayo
kutokana na asili yake mbaya ambapo huweka nundu nundu uwanjani na kusababisha
mpira kukosa mwelekeo unaopaswa wakati ukichezwa katika uwanja husika.
Amezitaka timu za Mbeya City na Tanzania Prisons
kutojawa na hasira baada ya kuzuiwa kutumia uwanja huo kwa mazoezi badala yake
watambue kuwa uongozi wa uwanja una nia
ya dhati ya kuboresha miundombinu itakayosaidia timu hizo kucheza mpira mzuri
na wenye kuvutia.
No comments:
Post a Comment