Mkuu wa wilaya ya Kyela Thea Ntara(wa tatu kutoka kulia) akiwa na maafisa wa TMA na wadau wengine wa shughuli za kimaendeleo katika ziwa Nyasa.Wadau hawa walikutana mjini Kyela kupashana habari za ujio wa TMA katika ziwa Nyasa sambamba na kupeana uzoefu juu ya majanga ya ziwa hilo.
Kaimu mkurugenzi wa
huduma za ufundi za TMA Dk.Pascal Waniha akielezea namna TMA ilivyoona umuhimu wa kufikisha huduma zake kwa watumiaji wa ziwa Nyasa.
Wadau mbalimbali wa ziwa Nyasa wakiwemo wavuvi wakishiriki semina ya kupeana uzoefu juu ya majanga ya ziwa hilo.
Wanahabari kama anavyoonekana mwandishi wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo Solomon Mwansele ni miongoni mwa wadau ambao wametajwa kuwa na umuhimu mkubwa kwenye usambazaji wa taarifa zitakazotolewa na TMA juu ya utabiri wa hali ya hewa ndani ya ziwa Nyasa.
Mkuu wa wilaya ya Kyela
Thea Ntara akibainisha namna ujio wa TMA katika ziwa Nyasa ulivyoleta neema kwa watumiaji wa ziwa hilo
Mkurugenzi wa huduma za Utabiri za TMA Dk.Hamza Kabelwa akibainisha mikakati ya TMA katika utoaji taarifa za hali ya hewa.
HABARI KAMILI.
MAMLAKA ya Hali ya Hewa
Tanzania(TMA) imepeleka huduma zake katika wilayani Kyela lengo ni kusogeza
huduma ya upatikanaji wa taarifa za hali ya hewa kwa watumiaji wa ziwa Nyasa.
Kwa mujibu wa watumiaji
wa ziwa Nyasa wakiwemo wavuvi na wasafirishaji,kwa muda mrefu wamekuwa
wakilazimika kutumia njia za asili kubaini majanga yanayoweza kutokea ndani ya
ziwa hilo na wakati mwingine walilazimika kutumia taarifa zilizotolewa na
mamlaka ya hali ya hewa ya nchi jirani ya Malawi.
Wakazi wilayani Kyela
wanasema kutokana na changamoto hiyo madhara makubwa yamekuwa yakitokea ikiwemo
vifo vya wavuvi kutokana na vimbunga vilivyowakumba wakati wakiendelea na
shughuli zao ndani ya ziwa Nyasa.
Kaimu mkurugenzi wa
huduma za ufundi za TMA Dk.Pascal Waniha anasema mamlaka hiyo imeamua kuwafikia
watumiaji wa ziwa Nyasa kutokana na mahitaji yaliyopo.
Mkuu wa wilaya ya Kyela
Thea Ntara anasema sasa watumiaji wa ziwa hilo wako katika mazingira salama kwakuwa
kabla ya kufanya shughuli zao watapataa taarifa za uhakika juu ya utabiri wa
hali ya hewa.
No comments:
Post a Comment