MAJIMBO ya Mbeya mjini
na Mbeya vijijini huenda yakagawanywa na kuwa majimbo mawilimawili iwapo Tumea
ya taifa ya uchaguzi itaridhia maombi yaliyopendekezwa na wadau kwenye vikao
vya Ushauri vya wilaya vilivyofanyika jana.
Vikao vya kuyagawa
majimbo hayo vimefanyika kwa nyakati na tofauti kwenye ukumbi wa halmashauri ya
wilaya ya Mbeya ambapo kwa jimbo la Mbeya mjini wadau wamependekeza kuundwa kwa
majimbo mapya ya Iyunga na Sisimba huku Jimbo la Mbeya vijijini likipendekezwa
kuundwa kwa majimbo ya Mbeya na Isangati.
Akizungumza kwenye
kikao cha Ushauri cha wilaya,Mkurugenzi wa jiji la Mbeya Bwana Musa Zungiza amesema
mapendekezo ya mgawanyo wa jimbo la Mbeya mjini yanazingatia maeneo ambayo
awali yalikuwa ni tarafa.
Bw.Zungiza amesema
katika Tarafa ya Iyunga ambayo sasa inapendekezwa kuwa jimbo kuna kata 21 na
mitaa 116,iinakadiriwa kuwa na wakazi 327,122 hadi kufikia Julai 2015 idadi
aliyosema inakidhi vigezo vya tarafa hiyo kuwa jimbo.
Kwa upande wa tarafa ya
Sisimba inayopendekezwa kuwa jimbo la Sisimba amesema ina kata 15 inayokadiriwa
kuwa na wakazi 106,264 kufikia Julai mwaka huu.
Naye mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri Bibi Upendo sanga amesema jimbo la Mbeya litakuwa na
kata 11 zinazokadiriwa kuwa na jumla ya wakazi 107,349.
Bi.Sanga amesema jimbo
la Isangati lenye kata 15 zinazokadiriwa kuwa na jumla ya wakazi 221.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment