Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Saturday, September 3, 2011

RC aagiza walionyanyasaa wananchi kwa kukosa vyoo watimuliwe



MKUU wa mkoa wa Mbeya Bwana John Mwakipesile ameuagiza uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe kuwachukulia hatua za kisheria watumishi waliokwenda kuwanyanyasa wananchi katika kata Kisiba kwa madai ya kufanya msako wa wakazi wasiokuwa na vyoo.

Kwa mujibu wa mkuu huyo wa mkoa watumishia hao ambao ni maafisa wa afya wakishirikiana na baadhi ya watendaji katika kata hiyo waliendesha zoezi hilo mapema wiki hii ambapo amelalamikia taratibu walizokuwa wakizichukua dhidi ya wasio na vyoo ikiwa ni pamoja na kunyang’anya mali zao.

Ameyasema hayo leo katika kikao maalumu cha baraza la madiwani kilicholenga kujadili taarifa ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali CAG.

Bwana Mwakipesile amesema maofisa hao waliwatoza fidia za aina tofauti wananchi hao wakiwemo wazee wasiojiweza pasipo kuwapa stakabadhi hali inayodhihirisha kuwa zoezi hilo lililenga maslahi binafsi.

Ametoa siku hadi jumatatu ya wiki lijalo kupelekewa majina ya maofisa hao ofisini kwake ikiwa ni pamoja na hatua zilizochukuliwa dhidi yao.

No comments:

Post a Comment